Dstv Tanzania

KONGAMANO LA MAADILI LAFAANA MKOANI NJOMBE PIA WAMETOA MSAADA WA CHAKULA KITUO CHA AFYA NJOMBE MJINI


Na.Titho Stambuli

Jumuiya ya wazazi mkoa wa Njombe imeendesha kongamano la maadili ili kuweza kuhakikisha jumuiya iko salama na kulinda maadili ya jamii yetu .

Mratibu wa kongamano hilo ambaye ni katibu wa wazazi mkoa wa Njombe   Ndugu Lucas Nyanda ameweza kumudu kuhakikisha Kongamano hilo lililofanyika ndani ya ukumbi wa turbo .


Lengo la kongamano hilo ni kuhakikisha wazazi wanaweza kulinda na kuwafundisha maadili mema watoto na kuhakikisha tamaduni za kiafrica zinalindwa kwani ndio zenye kuweza kuhakikisha usalama wa Africa.

"Tumefanya kongamano ili kujua chanzo cha mmomonyoko wa maadili ,Madhara na mikakati ya kudhibiti mmonyoko wa maadili "

Akihutubia mkutano huo katibu wa wazazi amesema bila maadili thaman ya mwafrika hakuna ,uchumi hakuna na migogoro itakuwa mingi bila sababu na nguvu kazi ya taifa itapotea ,tunawategemea vijana kuhakikisha nchi inakwenda .

Naye mgeni rasmi wa kongamano hilo amewaasa wazazi kuona mbali juu ya swala zima la maadili bila maadili usalama utakuwa rehani ili mwafrica athaminiwe ni Lazima kulinda maadili ya taifa letu .tuwadhibiti watoto wetu na ulevi ,uvivu na kufanya mambo yasiyo na tija katika jamii ,kwani vyote hivyo vinamfanya kijana kupoteza hata dira ya uchumi kwakuwa usalama wake ni mdogo na hata kusababisha uhai wake .

Ili uchumi uinuke na ulinde uchumi wako ni lazima tahadhari iwepo juu ya utandawazi juu ili kuweza kunusuru jamii yetu .Hivyo amewataka wazazi kuhakikisha maadili wanalinda na kuwafundisha watoto wao namna gani ya kuhakikisha watoto wanakuwa na maadili mema kwa maslahi ya taifa letu.

Na pia baada ya kuhitimisha kongamano hilo wameweza kutoa msaada wa chakula katika kituo cha Afya Njombe mjini kwa wagonjwa ,jumuiya ya wazazi imeona ni vyema wakatumia siku hiyo kula pamoja chakula na wagonjwa katika kituo hicho.

Akizungumza na mtandao huu katibu wa wazazi mkoa wa Njombe Ndugu Lucas Nyanda  amesema hii ni ishara ya upendo na ukarimu wetu watanzania,tumeona ni vyema baada ya kongamano tupate chakula kwa pamoja na kuwafariji wagonjwa na kuwaombea wagonjwa waweze kupona haraka na warejee katika majumu yao ya kulitumikia taifa letu.

Picha Zaidi



Hakuna maoni: