Dstv Tanzania

MKITAKA KUJUA UMUHIMU WA POLISI NCHINI WAFUNGE VITUO JAPO SIKU MOJA "katibu Mwenezi CCM mkoa wa Njombe "

Na.Titho Stambuli.

Mgeni rasmi katika kongamano la maadili mkoan Njombe ambaye ni katibu mwenezi ccm mkoa wa Njombe Erasto Ngole ,amesema kwamba ili watanzania tuamini na tutambue kuwa maadili yameharibika ni lazima siku moja tufanye jaribio la kufunga vituo vya polisi nchini halafu tupime tuone tutaweza kuheshimiana na kulinda maliza zetu..

Akihutubia wajumbe wa kongamano hilo amewataka kuhakikisha wanalinda maadili ya taifa letu na familia zao ,usalama wa taifa hili unategemea maadili bila maadili Ndugu zangu hakuna kitakachofanyika itakuwa ni kuvurugana .


Juhudi zote zinazofanywa na Raisi wetu Dokta magufuli haziwezi kuendelea bila watu kuwa na maadili maana usalama utakuwa mdogo na vitu vingi vitaharibiwa na kama tumeshindwa kujiheshimu ni vyema tukawaacha polisi wakatudhibiti sisi na Mali zetu ili nchi inyooke na kuhakikisha usalama wetu.

Hakuna maoni: