MBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE AWAPONGEZA WAPINZANI WANGING'OMBE,KWA KUTOKUWEKA MGOMBEA KWA KUTHAMINI KAZI NZURI INAYOFANYWA NA MH .RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Mbunge machachari wa vitimaalumu kutoka mkoa wa Njombe Bi Neema Mgaya ,mzaliwa wa jimbo la wanging'ombe ameonekana kuwapongeza wapinzani kwa kutokuweka mgombea katika uchaguzi mdogo kata ya Kata ya Itulahumba -Wilaya ya wanging'ombe.
Mbunge huyo mwenye busara na hekima ya aina yake ametafsiri kuwa kitendo hicho ni wapinzani kukubali kazi nzuri inayofanywa na Mh Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John pombe Magufuli ,kwa kuwajali wanyonge ,kupinga Rushwa ,Kujenga miundo mbinu mizuri na kusimamia Raismali za taifa hili kwa maslahi ya kila mtanzania na kila mmoja wetu kunufaika na keki ya taifa hili .
Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao wa stambulinews ameonekana kufurahishwa na kuwapongeza wapinzani kwa kuamua kutokusimamisha mgombea ili kumpisha mgombea wa ccm kupita bila kupingwa kuonyesha kumuunga mkono Raisi wetu kwa juhudi kubwa anazozifanya.
"Kwa Mimi ninawapongeza kwa kuamua hivyo pia nampongeza mheshimiwa Raisi kwa kuwa kazi anazozifanya wapinzani wanazikibali na ndio maana hawaoni sababu ya kuipinga ccm"
Mh Neema Mgaya amepongeza viongozi na watendaji wa ccm-Njombe kwa kuwatuliza vyema wanaccm na kushirikiana na serikali kwa kuweza kuwatumikia wananchi mpaka wapinzani wameanza kukubali kuwa ccm ipo kazini kwa maslahi ya watanzania na wameona hakuna haja ya kukipinga chama cha mapinduzi.
Mheshimiwa Neema Mgaya amewapongeza na kuwashukuru wapinzani Njombe kwa kujitoa na kukiacha chama cha mapindizi kipite bila kupingwa na kuokoa gharama na kuharakakisha maendeleo kwa wananchi wa kata ya Itulahumba.
Mhe Neema amesema watu wa Wanging’ombe ni watu wapekee sana ambao wakiamini kitu ni kizuri wanakiamini kwa nguvu zao zote.
Na ndio maana wakati uchaguzi ulipofika kwa kazi nzuri inayofanywa na Mhe Rais Dr Magufuli mwkt wa CCM Taifa , mgombea wa udiwani kupitia chama cha ACT hakuona sababu ya kugombea na badala yake a kaamua kuunga mkono chama cha mapinduzi.
Na Hii ndio sifa ya watu wa Wanging’ombe kizuri watakipenda na kukithamani, hivyo basi naona upendo mkubwa wa wananchi wa Wanging’ombe kwa CCM hususa Mhe Rais wetu mpendwa Dr Magufuli.
Lakini upendo huu umekuja kwa kwa kazi nzuri anaiyoifanya Rais wetu Mhe Dr Magufuli ya kuwaletea Maendeleo wananchi wa Wanging’ombe na watanzania kwa Ujumla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni