|
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James Akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve mapema leo walipowasili mkoani Iringa,Katikati yao ni Katibu mwenezi wa CCM-Njombe Erasto Ngole. |
Na,Titho Stambuli,Iringa.
Kamati hiyo Imeongozwa na mwenyekiti wake UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve ,Katibu UVCCM-Njombe Sure Mwasanguti ,Katibu hamasa na Chipukizi Johnson Mgimba,Mjumbe wa baraza uvccm taifa kutoka Njmbe Thobias omega na mjumbe wa kamati ya utekelezaji Joyce sigala wakisindikizwa na Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe.
|
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Kheri James Akiwa katika Kikao na Viongozi wa UVCCM Mkoa wa Iringa. |
Viongozi hao mapema Alfajiri walianza safar kuelekea Iringa kumpokea Mwkt UVCCM taifa Ndg Kheri Denis James ambaye amewasili Iringa kwa ajili ya kuimarisha jumuiya na kushiriki kampeni za Udiwani kata ya Mwangata.
|
Wakwanza kushoto ni katibu wa
itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiteta jambo la
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Njombe Nehemia Tweve.
|
Viongozi hao waliofunga safari kwaajili ya kuonana na Mwenyekiti huyo kwanza kabisa kumpokea na kumkaribisha ,na kumpa taarifa ya mikakati ya kuzidi kuimarisha uvccm Njombe na mwelekeo wake kwa maslahi ya UVCCM mkoa wa Njombe na taifa na pia ccm kwa ujumla .
|
Viongozi wa UVCCM Mikoa ya Njombe na Iringa wakiwa katika Picha ya Pamoja. |
Ujio wa kamati ya utekelezaji mkoa wa Njombe imeleta amsha amsha na furaha kwa wenyeji kwakuwa wao kama mkoa mama wanafurahi kuona ushirikiano wanaoupata kutoka katika mkoa ambao ulizaliwa kwao.
|
Katibu UVCCM Mkoa wa Iringa(Kushoto) James Magego akiteta jambo na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti |
Licha ya kufanikisha mapokezi hayo kwa kushirikiana na wenyeji wao viongozi hao wanatarajia kukutana na kuifanya kikao na mwenyekiti wa UVCCM taifa ,kesho mkoani Iringa,Huku kikao hicho kikiwa kimelenga kuimarisha jumuiya mkoa wa Njombe, kuimarisha mahusiano kati ya Iringa na Njombe kwa kubadilishana uzoefu na pia kuhakikisha ccm inakuwa imara kwa maslahi ya watanzania.
Viongozi hao kutoka mkoani Njombe wameweza kuhudhuria mkutano ambao uliandaliwa mwenyekiti kuwahutubia vijana wa Iringa Mjini .
|
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve akiteta jambo na Seck Kasuga Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa. |
Mwenyekiti Kheri Denis James amewahutubia vijana wa Iringa kutembea kifua mbele kwani ccm ipo tayari kuwapigani kwani ccm inatambua vijana wanahitaji uhuru wa kufanya kazi ,amewataka viongozi wa ccm kushughulika na kero za vijana wasinyanyaswe,na badala yake wawe sauti ya wanyonge.
"Tunahitaji viongozi wa ccm kuisimamia serikali vilivyo kwa maslahi ya watanzania wahakikishe wanfuatilia utekelezaji wa ilani kwani kodi za wananchi zimekuwa zinatakiwa zitumike vilivyo".
Ameyasema hayo mjini Iringa lkn pia amewataka viongozi wa Njombe waliohudhuria mkutano huo kuyafanyia kazi hayo kwani hayo ndio malengo ya ccm.
|
Katibu mwenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole. |
Amewatoa hofu pia kuwa serikali ya ccm haitampendelea mtu ambaye hawajibiki ila itampendelea yoyote atayewajibika hivyo amewataka watendaji na vijana kuwajibika vilivyo na si kusubiri kupewa kila kitu.
|
Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti UVCCM (M)NJOMBE Nehemia Tweve,Mjumbe wa baraza UVCCM taifa kutoka Njmbe Thobias Omega,Katibu UVCCM-Njombe Sure Mwasanguti. |
Viongoz wa UVCCM kesho watakutana na Mwenyekiti UVCCM taifa mjini Iringa
......endelea kutufuatiliaa
Zaidi Tazama Picha Hizi Hapa Chini.
|
Eddo Kumwembe (katikati)Katibu mwenezi Wilaya ya Iringa akiwa na Mwenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole na Kulia ni Balozi wa Shule za Wazazi mkoa wa Njombe Titho Stambuli. |
|
Said Lubeya Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini Akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Njombe Nehemia Tweve. |
|
M/Kiti UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve |
|
Sure Mwasanguti Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni