KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM MKOA NJOMBE YAKUTANA NA M/KITI UVCCM TAIFA KHERI JAMES
Mtoto kwa mama hakui......
Na Titho Stambuli,Iringa.
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM kutoka mkoa wa Njombe
wamefika mkoa wa Iringa kuonana na mwkt UVCCM
taifa Comrade Kheri Denis James na kufanya mazungumzo yenye kuzidi kujenga na
kuimarisha uhai wa jumuiya ndani ya mkoa wa Njombe .
Wajumbe kutoka mkoa wa
Njombe wakiongozwa na Mwkt wa Mkoa wa Njombe Cde-Nehemia Tweve,Katibu UVCCM
mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti ,Katibu
hamasa na chipukizi Mkoa wa Njombe Johnson Elly Mgimba ,Lkn pia wajumbe
hao wamesindikizwa na Katibu Mwenezi Erasto Ngole.
Viongozi wa UVCCM Mkoa wa Njombe na Iringa wakiwa katika kikao kazi na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James Mapema Leo Kilichofanyika Mkoani Iringa. |
Wajumbe wameweza kuketi na Mwkt UVCCM taifa kumueleza hali
ya UVCCM mkoa wa Njombe na Mwelekeo wake
katika kuifanya jumuiya hiyo kuwa na Nguvu sana kwa maslahi ya ccm na taifa
hili .
Hapana shaka juu ya uwezo wa Mwkt UVCCM mkoa wa Njombe na Katibu wake
Mwasanguti Licha ya kumueleza Mwkt wako salama ,Lkn bado wanahitaji ushirikiano
wa hali ya juu katika kuhakikisha Mkoa
mama unakuwa karibu na Njombe ili kuifanya ccm kuwa na Nguvu Nyanda za juu
kusini.
Zaidi Tazama Matukio katika Picha hapa Chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni