KUNA UTOFAUTI MKUBWA WA KAULI BAINA YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA
Leo ninawaletea nukuu kadhaa za viongozi wa juu kabisa wa
Upinzani na CCM kwa Jamii alafu utaweza tafakari ni viongozi wa namna gani
wanapaswa kuendelea kuaminiwa na wananchi wa Tanzania
Nitachagua viongozi wa juu kabisa mmoja kutoka vyama vya
CCM, CHADEMA NA ACT ambapo kila mmoja nitamtolea nukuu ( Kauli) tatu ambazo
alikiwisha wahi kuzisema katika jitihada za kukitambulisha Chama Chake kwa
Jamii.
Nianze na Kiongozi wa CHADEMA;
Ndg. Freeman Aikael Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa
CHADEMA,
"Viongozi wangu mnapohutubia, wananchi hawa, msihutubie
kwa furaha, muhutubie kwa kuwajaza wananchi hasira". Nov 2017 Ndalambo.
"Tuunganishe nguvu ya Umma staili ya Libya, Misri,
mambo kama ya Libya na Misri tunayahitaji, wanasema Mbowe ni Mchonganishi,
kweli mimi ni mchonganishi". Aug 2016 Mwanza.
"Suluhu ya Nchi hii ni lazima tubebe majeneza hata mia
mbili ili tupate suluhu ya matatizo yetu". Feb 2018 Kinondoni.
Ndg. Zitto Zuberi Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini na
Kiongozi Mkuu wa ACT
"Ni makosa makubwa, Tanzania kutangaza ushindi katika
mapambano ya madini dhidi ya Mabeberu Accacia". Okt 2017 Dar Es salaam
"Tumechoka kutumbua majipu (Kufukuza wezi), kwa sababu
sisi hatuli usaha, tunataka Tanzania itangaze baa la njaa". Machi 2017.
"Nchi nzima inajadili Suala ya la Makinikia, kwangu
mimi hili ni suala dogo sana." Mei 2017 Dar Es Salaam.
Ndg. John Pombe Magufuli
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania.
"Tufanye kazi kwa kujitoa, tuwahudumie wananchi, hii
kazi tumepewa na mungu, na tutawajibika kwa jambo tunalolifanya kwa
Watanzania". Aug 2018
"Tunataka kujenga Tanzania mpya yenye uchumi wa kati,
mzuri na maendeleo makubwa kupitia ushirikiano na nchi za nje na Sekta binafsi". Julai 2017
"Mimi nachukia wezi na kwa kweli wezi watakoma tu, awe
mwizi wa Tanzania, awe wa Ulaya, awe anatoka mashariki, magharibi, kaskazini
ama kusini mwizi ni mwizi tu, tutaendelea kubana mianya yote ya wizi". Jan
2017
Kiongozi hupimwa na kauli zake, yanafuata matendo. Lakini
pia kuna msemo usemao limtokalo mtu ndio limjaalo moyoni mwake.
Leo nitaachia hapo kuacha tafakuri kwenu.
Mimi mwandishi wenu
Said Said Nguya
Saidnguya@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni