MSAFARA WA KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM NJOMBE NA KATIBU MWENEZI MKOA WA NJOMBE, WAKUTANA USO KWA USO NA NAIBU SPIKA NJIANI NYORORO .
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson Akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole walipokutana Njiani Mchana Wa Leo wakati wanarejea Njombe. |
Msafara huo uliotokea Mkoani Iringa ziara ya kikao kazi kukutana na Mwenyekiti UVCCM taifa Kheri Denis Names, walipokuwa wanarudi wamekutana njian na naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Tulia Ackson.
Kamati hiyo iliyokuwa inaongozwa na Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Njombe Nehemia Tweve, katibu uvccm mkoa Sure Mwasanguti, Mjumbe wa Baraza kuu uvccm taifa thobias Omega na mjumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa Joyce sigalla wakiwa wameongozana na katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Cde -Erasto Ngole wamesalimiana na kiongozi huyo na kutakiana kazi njema viongoz hao na pia kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya bungeni na kusaidia utekelezaji wa Irani yaCCM
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve. |
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson akisalimiana na Mjumbe wa Baraza kuu uvccm taifa Thobias Omega |
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson Akiwa na mjumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa Joyce sigalla |
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson (katikati)akiwa na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti (Kushoto) pamoja na Balozi wa Shule za Wazazi mkoa wa Njombe Titho Stambuli |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni