Dstv Tanzania

BALOZI WA NMB BANK COMRADE AWARD MPANDILA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WABENKI YA NMB TANZANIA.


Kutoka Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB kutokea makao makuu ya Benki Hiyo Nchini Uholanzi,Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dsm Badro Idd ,Balozi wa NMB Tanzania Award Mpandila,Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya NMB Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr George Mulamula
Na,Titho Stambuli.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar Es Salaam Badro Idd Akiwa ameongozana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Hiyo akiwemo Mjumbe Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr George Mulamula,Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB kutokea makao makuu ya Benki Nchini Uholanzi Bi.Christine ,Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kariakoo Jonathan Kombe  amemtembelea na Kufanya mazungumzo na mjasiliamali ambaye pia ni  Balozi wa Benki ya NMB Tanzania Award Mpandila.
Balozi wa Benki ya NMB Tanzania Award Mpandila wa kwanza kushoto akiwa na Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya NMB Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (Katikati) na  Mjumbe kutokea makao makuu ya Benki Hiyo Nchini Uholanzi (Kulia)
Baada ya mazungumzo na wajumbe hao Balozi huyo amesema anamshukuru Mungu kwa Kutembelewa na wajumbe hao.

‘’Namshukuru Mungu wa mbinguni siku ya Leo nimetembelewa na kufanya mazungumuzo na bord member wa bank yetu pendwa Nmb akiwa amejumuika pamoja na bord member anayewakilisha serikali ya Tanzania‘’ amesema Mpandila.

Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya NMB Kutoka makao makuu ya NMB Uholanzi Akisain Kitabu cha Wageni.

Aidha Mpandila amesema "Kipekee niwashukuru saana hawa wakurugenzi kutambua umuhimu wakushuka hadi  nchini kwetu kuja kusikiliza changamoto zetu"
Balozi wa Benki ya NMB Tanzania Award Mpandila Akiwa katika Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Tanzania,Mwenye Shati la Bluu ni Meneja Tawi la Kariakoo Jonathan Kombe

Aidha amewapongeza kwa kusikia kilio cha wateja kwa kukubali kwao kuwapunguzia riba katika Mikopo.

"Pamoja na pongezi nimewaomba ili kuweza kupunguza foleni ya kwenye matawi yetu nivyema kuongeza Nmb wakala nchi nzima’’amesema nakuongeza" Wamekubali ya kwamba wamejipanga kuongeza NMB Wakala kutoka 3000 za sasa wataongeza hadi kufikia 6000’’
Mpandila Licha ya kuwapongeza ameahidi kuendelea kufanya kazi vizuri ya  kuwaeleza watanzania uzuri wa bank pendwa  ya NMB.

Hakuna maoni: