Dstv Tanzania

MAKAMU MWENYEKITI CCM TANZANIA BARA AUNGURUMA KATA YA ISAPULANO-MAKETE,KUHAKIKISHA CCM INAPATA USHINDI WA KISHINDO.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Mh.e Philip Mangula akimnadi mgombea udiwani kata ya Isapulano Wilayani Makete Mchana wa leo

Na.Titho Stambuli

Makamu mwenyekiti Tanzania bara Mzee Phillip Mangula ametinga wilayani makete kuhakikisha CCM inashinda ushindi wa kishindo Katia kata ya Isapulano.

Makamu mwenyekiti  Mzee Mangula ameongozana na viongozi Ngazi ya mkoa Mwenyekiti Mzee Jassery Mwamala,Katibu ccm mkoa Hosea Mpagike ,Katibu Mwenezi Hosea Mpagike,Katibu wa wazazi Mkoa Lucas Nyanda ,Mwkt uvccm mkoa Nehemia Tweve ,katibu uvccm mkoa Sure Mwasanguti ,kada kutoka Songwe na Afisa kutoka ofisi ya vijana salumu chone.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula akiwa na Mgombea Udiwani wa Kata ya Isapulano
Ngoma nzito kwa wapinzani kwani makete imezidi kufikiwa na wa geni kutoka sehemu mbalimbali ,na Leo amefika mgeni wa kitaifa mzee phillip mangula kwaajili ya kuongeza Nguvu kuhakikisha CCM inashinda licha ya wenyeji wake kuwa na mikakati yao lkn pia vigogo wa ccm wamezidi kuendelea kuwakumbatia  wapinzani hali inayochangia wapinzani kuzidi kuchanganyikiwa na wanachama wao kuhamia ccm kila kukicha na leo Mh mangula amewapokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani.
Mbunge wa Jimbo la Makete Pr.Norman Sigala King akimnadi Mgombea udiwani kata ya Isapulano
Akiwahutubia wananchi wa makete kata ya Isapulano amewaeleza wananchi hao kutambua kazi zinazofanywa na serikali ya ccm ndani ya wilaya ya makete na kata ya isapulano ,ujenzi wa barabara,hospital pamoja na madawa na wataalamu ,ujenzi wa shule ,maji na vijiji 51  vimepata umeme wa REA ,na bado miradi mingine inaendelea kutekelezwa.

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akimnadi Mgombea Udiwani kata ya Isapulano
Hivyo amewataka wananchi wa kata hiyo kuamua maamuzi sahihi ambayo yatawafanya waende kwa kasi zaidi na sio kuweka kigingi katikati na pia itakuwa ni shukrani kwa ccm na kumpongeza Raisi wetu dokta John pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na kuiongoza vyema serikali ya  CCM

"ninawaomba wananchi wa kata ya isapulano mfanye maamuzi sahihi kwan maendeleo yanakuja kwa mnyororo ambao umepangilika hivyo hata serikali ya ccm inahitaji kuwa na viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wote ccm ili kutokuwa na kizuizi katika katika mlolongo mzima wa kuleta maendeo maana mkichagua upinzani kila kitu wanapinga hivyo hamna sababu ya kuwachagua tena"
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve akimuombea kura mgombea udiwani mbele ya wananchi wa kata ya Isapulano
Na pia amempongeza diwani aliyeamua kurudi ccm kwani amefanya maamuzi sahihi kwa kuwa hata kuwa na upinzani katika baraza la madiwani na kupata nguvu ya kuharakisha maendeleo katika kata ya isapulano. 

Lakini pia amewataka kuepuka hasara kwa kuwachagua wapinzan kwani mwisho wa siku kila mtu anarudi ccm kwakuwa kule hakuna siasa ya kweli na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi hivyo wakataeni unganeni na ccm Katika kuharakisha maendeleo.
Katikati ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Makete  Nehemia Sanga
Mh Mangula amewakumbusha wananchi hao kuwa ccm hawana uadui na upinzani ila wanauadui na ujinga, maradhi na umaskini hao ndio maadui zetu, na ndio mipango ya ccm tangu tupate uhuru, Hawa wapinzani wanawapotosheni siasa zao ni fujo, matusi na hawana mipango ya kimaendeleo .
Mamia ya Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapanduzi Tanzania Bara Philip Mangula.
Hivyo amewaomba wananchi hao kudumisha amani kwani bila amani Hakuna maendeleo hivyo tuwaepuke wanasiasa wanaoweza kusababisha machafuko ya kisiasa na kuacha shida katika jamii zetu.
Kushoto ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti akiwa na Mkuu wa wilaya ya Makete  Veronica Kessy
Amewataka wananchi hao na wanasiasa kuwa na hofu ya Mungu ili kuepuka kuhatarisha amani ya nchi yetu, kila mmoja aape kwa dini yake ili kumkabidhi Mungu familia zetu,na nchi. 

"Ndugu zangu bila hofu ya Mungu tutaharibu amani ya nchi yetu na tusimame imara na tuwe na hofu na wanasiasa wanaotaka kuhatarisha amani na tuwakatae kwa maslahi ya taifa letu.

Zaidi Tazama Matukio kwa Picha hpa chini.



Hakuna maoni: