Dstv Tanzania

BALOZI WA BENKI YA NMB TANZANIA AWARD MPANDILAH APONGEZA USHINDI WA RAISI EMMERSON MNANGAGWA WA ZIMBABWE,AWASIFU WANACHI KWA KUFANYA UCHAGUZI WA AMANI NA UTULIVU.


Na.Erasto Mgeni.

Balozi wa Benki ya NMB  Tanzania na ambaye pia ni Mjasiliamali Cde-Award Mpandila amempongeza rais mteule wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa kwa kuchaguliwa kuliongoza Taifa hilo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii.
 
Mnangagwa ameshinda uchaguzi huo baada ya kujikusanyia asilimia 50.8 ya kura huku Nelson Chamisa wa Muungano wa chama kikuu cha upinzani (MDC) akipata asilimia 44.3.


Katika ujumbe aliouchapisha kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Cde-Award Mpandila ‘’Hongera sana Hon.Mnangagwa kwa Ushindi’’


Hali Kadhalika Mpandila amewapongeza Pia Wananachi wa Taifa hilo kwa Kufanya Uchaguzi wa amani na Utulivu.


“nichukue Fursa hii kuungana na rafiki zangu wa Zimbabwe kwa kufanya uchaguzi wa amani na utulivu katika taifa lao na kumpata kiongozi mpya ambae kwa mara ya kwanza tokea uhuru ndio wanafanya uchaguzi”ameandika Mpandila katika ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter.


Katika Chapisho hilo Mpandila ameambatanisha na picha akiwa na marafiki zake wa Zimbabwe kama inavyoonyesha hapa chini.

Hakuna maoni: