Dstv Tanzania

KATIBU WA CCM WILAYA YA MAKETE AWAVISHA WAPINZANI KINGI YA 7 KWA 7,HUKU MAKAMU MWENYEKITI CCM TANZANIA BARA PHILLIP MANGULA AKIPIGILIA MSUMARI WA MWISHO.


Katibu wa CCM wilaya ya makete Comrade Akyoo Akimnadi mgombea Udiwani Kata ya Isapulano
Na.Titho Stambuli.

Kumekucha kata ya Isapulano kampeni upande CCM zimenoga huku wapinzani wakilizwa.

Katibu wa CCM wilaya ya makete Comrade Akyoo ameonekana kuitendea vyema nafasi ya ukatibu pale unapoona kila kata wanasema naaam huyu ndiye katibu.


Hayo yamejidhihirisha Live katika kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea ndani ya wilaya yake kata ya Isapulano pale aliposepa na kijiji kwenye mkutano wa kampeni, siku hiyo hiyo chadema na wao walikuwa wanasubiri muda ufike wafanye mkutano jambo hilo halikufanikiwa pale walipokuta wamepata watu 7 na viongoz saba jumla kumi na nne ,na mkutano ukaahirishwa hapohapo.

Jambo Hilo limewamaliza Nguvu za kuendelea na kampeni wababaishaji hao kwakuwa wananchi wamewakataa kabisa katika kata hyo kwani wamewauliza swali gumu kwamba .

"Tulikupa mtoto umlee umeshindwa sasa unataka nini tena" hali iliyopelekea wapinzani kushindwa kupata watu na kuamua kuahirisha kufanya kampeni kwasababu ni fedheha na aibu.

Huku ccm ikisepa na kijiji kwa kuwa na maelfu ya wananchi waliokusanyika kwaajili ya mkutano huo na ukichagizwa na makamu Mwenyekiti CCM Tanzania bara na kupambwa na burudani huku wanenaji wazuri wa kampeni wakiwepo na kupanda kutoa dozi jukwaani vichwa kama Sure.

Mwasanguti, Erasto Ngole, Lucas Nyanda na kada kutoka songwe sadock Mwanda na comrade Nehemia Tweve walipolindima jukwaani na kuvuta umati mkubwa kwa watu na umakini mkubwa na burudani kutoka vikundi mbalimbali.

Hayo ni moja ya mafanikio ya katibu wa ccm wilaya ya makete kudhihirisha kwamba ameweza kumudu na kufanikiwa kuwafanya watu waishi katika imani na ccm.
Akizungumza na mtandao huu ni kwamba anawashukuru sana watendaji kuanzia ngazi ya chini mabalozi ,makatibu na viongoz wote kwakuwa wamekuwa wakimpa ushirikiano wa kutosha na ndio maana anapata Nguvu ya kujivunia na hivyo kukifanya chama cha mapinduz kuwa imara ndani ya makete .

Kwa mshikamano huo anauhakika ccm itashinda kwa kishindo tena kwa asilimia kubwa kazi itakayo kuwa imebaki ni kuisimamia serikali kuhakikisha inatekeleza ilani ya ccm vyema ili wananchi waweze kuendelea kuwa na imani na ccm na kubaki na msimamo ndani ya ccm.


"Mimi kwangu najivunia kuwa na ushirikiano wa hali ya kuu namna hii kwa kuwa inanifanya nifanikiwe kuendelea kukipa Nguvu chama cha mapinduzi"


Wapinzani waje tuu ccm maana watapata aibu kila kukicha hao watu saba waliowapata ni wengi kuna siku watajikuta wapo vionvozi peke yao warudi tuu nyumbani kumenoga .....
 

CCM Hoyeeeeeeee

Tukutane Tarehe 12/08/2018 na kichinjio cha kuwachinjia chadema

Hakuna maoni: