Dstv Tanzania

UWT NJOMBE WAKABIDHIWA GARI NA MAKAMU MWENYEKITI CCM TANZANIA BARA PHILLIP MANGULA,PIA AMEGAWA KADI ZA CHF KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, ASHUHUDIA NA SACCOS YA UWT


Na,Titho Stambuli.

UWT wilaya ya Njombe imezidi kupata mafanikio ya kitaasisi baada ya kufanikiwa kununua gari lao kwaajili ya shughuli za UWT na uanzishwaji wa SACCOS ya wanawake na kuwalipia Kadi za CHF wanafunzi 84 wanaoishi Katika mazingira magumu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula akiingia katia Ukumbi wa UWT-Turbo Njombe Mjini
Licha ya kuwa wanawajibika ipasavyo kuhudumia na kusaidia na pia wamekuwa na jukumu la kuandaa viongozi wakina mama hawa mahiri  katika swala zima la kuhakikisha uchumi unakuwa imara na kwa wanachama wao na na jumuiya kwa ujumla,kwani jumuiya imejidhihirisha kuwa ni imara kwa kuibua fursa mbalimbali kwa maslahi ya jumuiya na ccm kuwa imara.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula Kushoto akisalimiana na Katibu wa UWT Wilaya ya Njombe Grace Haule.
Jumuiya hyo iliyochini ya mikono salama ya Mwenyekiti wake Bi Angela Mwangeni na Katibu wake mahiri kabisa Bi Grace Haule ambaye ameonyesha uwezo wa hali ya juu na ubunifu katika kuhakikisha jumuiya inakwenda.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe Angela Mwangeni
Mh Makamu mwenyekiti  wa CCM Tanzania Bara Phil Mangula amewahutubia wanachama wa UWT na wanachama waliohudhuria tukio hilo  amewapongeza kwa hatua nzuri waliojiwekea ya kusimama imara na kuweza kuonyesha mafanikio ambayo kila mmoja anayaona hakika ni jambo la kupongezwa na kweli akina mama wa ccm ni jeshi kubwa.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe Rosemary Lwiva
Mangula amevutiwa pia na UWT kuanzisha SACCOS na kukabidhi kadi za CHF kwa wanafunzi 84  kwakuwa ni jambo jema ambalo linakwenda kugusa maisha ya watu hasa hili la watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwakweli Mungu awatie nguvu kwani ni kazi ya Mungu mmefanya.
Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Erasto Ngole.
Aidha Mh Mangula amechangia shillingi Million moja kwaajili ya service ya gari hyo mpya ya UWT ili iweze kufika kuwasaidia kuwahudumia walengwa na Mwisho amekabidhi cheti cha SACCOS Kama ishara ya uzinduzi wa SACCOS Hiyo
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti
Mwisho Kabisa amekata utepe wa gari na kupanda Kama ishara ya uzinduzi wa gari hilo na Tatar kwa uzinduzi na tayar kwa matumizi.
Baadhi ya Wajumbe wa Balaza la UWT Wilaya ya Njombe
 Zaidi Tazama Picha hapa Chini.

Hakuna maoni: