Dstv Tanzania

MDAU WA ELIMU JOHNSON MGIMBA AHUDHURIA KIKAO CHA TATHMINI YA ELIMU LUDEWA CHA WARATIBU, WAKUU NA WALIMU WAKUU WA SHULE KILICHOITISHWA NA MKUU WA WILAYA

Mkuu wa Wilaya Ludewa Mh.Andrea Tsere amemtambulisha ndugu Johnson Elly Mgimba kwa wajumbe wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Ludewa tarehe 6/08/2018 ambao ni Wakuu wa shule,Walimu wakuu na Maofisa mbalimbali wa Elimu Wilaya wakiwamo Maafisa Elimu Kata Pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya kuwa ameuona moyo wa kijana huyu kati ya Vijana Ludewa walioamua kuhamasisha Elimu Ludewa kwa Hali na Mali na Mara zote amekuwa akitoa mchango mkubwa namna ya kuiboresha Elimu  kwenye vikao vya Elimu tangu kile kikao cha wadau wa Elimu mwezi februali.


 Mdau huyu wa Elimu ambaye Kijana mhitimu wa Elimu ya Juu kwenye maswala ya Uhasibu na Fedha alianza kwa kuelezea namna gani Elimu ni nguzo kuu kati ya nguzo katika kuleta Maendeleo kwa jamii.

Lakini pia aligeukia kuwashukuru Walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya na kusema wao ndio wameishika hatma ya kesho ya Ludewa kwakuwa wanaouwezo wa kuleta Ludewa mpya au kuleta Ludewa mfu kulingana na  ufundishaji wao.

Hivyo akiwasihi na kuwaomba Walimu kuwa mbali na kutimiza majukumu yao ya ajira lakini wanakila sababu ya kufanya kazi hii kwa moyo kwakuwa ndio wamebeba mafanikio ya Ludewa ambayo inatarajia kupokea miradi mikubwa ya kitaifa ikiwamo Nchunchuma na liganga kwakuwa miradi hii inahitaji wasomi wengi wazawa laa sivyo watakuja wageni kuajiriwa na wao wakabaki kuwa walinzi na wafagizi.

Aliwashukuru waratibu Elimu kata kwa taarifa nzuri walizowakilisha namna walivyoendesha makambi kwa kila kata na kusema kwakweli tunajivunia kwakuwa tumeanza kuona Mwanga wa Kesho nzuri ya Ludewa na Hakika matokeo ya Mwakani hatutakuwa tulipokuwa mwaka Jana.

Amewashukuru Walimu kwa ushirikiano na kwa moyo huo na akasema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kurudisha Hadhi ya Elimu ile iliyokuwepo zamani lakini pia Elimu ikirudi kule ilikokuwa zamani bila shaka hata hadhi ya mwalimu itarudi kama ilivyokuwa zamani.

Ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa mipango ya kuiboresha Elimu na akasema sehemu iliyobaki wazazi tunatakiwa kufanya sehemu yetu anaamini zamani wazazi wengi walipeleka watoto shule za private kwakuwa hawakuwa na imani na shule za serikali hivyo kwa sasa anaamini wazazi wameanza kurudisha imani kwenye shule hizi na hivyo Walimu ni swala LA kushikamana na wazazi na wadau mbalimbali wa Elimu.

Akiendelea kutoa pongeza na jitihada za Serikali yetu inayoongozwa na Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli akisaidiwa na wasaidizi wake DC kwa ngazi ya wilaya DED na wengine wote pamoja na Mh Mbunge pamoja na Bunge kwa namna wanaendelea kuishauri serikali kwakuwa tunaiona dhamira ya kuinua Elimu Tanzania inakuja hivyo Ludewa hatutakiwi kupitwa na hili mbali tupambane ndugu zanguni.

Kuhusu mfuko Maalumu wa Elimu Ludewa kama ambavyo na yeye aliahidi kushirikiana na Ofisi ya Wilaya kuuanzisha ili wadau wapate kuchangia kwa utaratibu utakaopangwa amesema mchakato huu upo mwishoni na soon wadau wataanza kuchangia.

Kama wadau wa Elimu tunajipanga kuwa Nyuma yenu na ndio moja ya jambo limenileta Ludewa kufuatilia hili pamoja na kusikiliza tathmini hii wapi tulipo tangu maazimio ya kikao kile cha wadau wa Elimu cha mwezi Februaly 2018.na kwa kweli  Mimi binafsi nikiwa ningali kijana mwenye nguvu nimejitoa kuhamasisha mfuko huu kwa wadau wengine kwakuwa tunaamini mfuko huu utasaidia baadhi ya bajeti za makambi yatakayofeli kufikia lengo lakini pia utasaidia kuwatafuta walimu wa Part time ambao kwa sehemu kubwa tutatumia vijana wetu wa chuo kikuu lakini na mipango mingine itakayoonekana inafaa na kukubaliwa katika kuiendeleza Elimu Ludewa.


Nitaendelea  kujitoa kwaajili ya  Elimu ludewa na ninaomba kwenye Mikutano ya Wazazi mnaweza kunishirikisha nikaja kutoa Elimu ya namna mfuko huu utatusaidia na kutuweka wanaludewa Pamona pia amesema kuna Kata imetoa ripoti kuwa  wazazi waligoma kutoa posho kwa walimu waliopo kwenye kambi amesema si kosa lao ila wamekosa Elimu ameomba wamwalike Mara moja kwenye kikao cha wazazi  hicho ili wakaelimishane ili kambi ijayo anaamini hawatafanya hivyo.

Akizungumzia kuhusu programm ya kuwapeleka vijana wa chuo kikuu kwenye Sekondary Ludewa anasema mpango huu umeshaanza na unaratibiwa na Umoja wa wanafunzi wanasoma vyuo vikuu unaoitwa LUSO huku wakisimamiwa na Group la watsap la Wilaya ludewa kupitia Admns wake na Kwa sasa program hii imekwishaanza na kuna vijana wamesharipoti kwenye shule zetu na kuna ushauri wa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na Afisa Elimu wa kuwapanga vijana ambao ni walimu wa Sanaa waende shule za Msingi kwakuwa sekondari uhaba sana ni walimu wa sayansi hili amelibeba na kwenda kuwakilisha kwa uongozi unaoratibu zoezi hili kwa sasa ili kuona kama yafaa tufanye marekebisho haya.

Amewapongeze wakuu wa shule zenye A level kwa matokeo mazuri hasa Mkuu wa Shule Ulayasi ambapo wahitimu waliofanya vizuri alipata kuwa mgeni Rasmi kwenye mahafari yao.

Mwisho alimshukuru Mh.DC kwa namna alivyoibeba Elimu Ludewa kwa moyo wa dhati na hivyo ameendelea kuwaomba wazawa na walimu na watendaji wote wa Idara ua Elimu tuwe na moyo kama wa Mh DC.



Titho Stambuli
Mwandishi wa Kujitegemea

Hakuna maoni: