MKUU WA MKOA WA NJOMBE ATEMBELEA BANDA LA WAKULIMA WA MITI NANE NANE MBEYA.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka Akisaini kitabu cha wageni katika banda la MUUNGANO WA VIKUNDI VYA WAKULIMA WA MITI TANZANIA. |
Katika Nyanda za Juu Kusini Mwa Tanzania Maadhimisho hayo ya Nane nane yamefanyika Mjini Mbeya katika Viwanja vya John Makangale Ambapo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho ya Nane nane Likiwemo banda la MUUNGANO WA VIKUNDI VYA WAKULIMA WA MITI TANZANIA.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa MUUNGANO WA VIKUNDI VYA WAKULIMA WA MITI TANZANIA |
Bwana Labani Mgimba Pia ameongeza kuwa wakuu wa Mikoa kutoka mikoa mingine nao walipata fursa ya kutembelea banda lao pamoja na mabanda mengine.
Kastory Timbula ni Meneja wa MUUNGANO WA VIKUNDI VYA WAKULIMA WA MITI TANZANIA pamoja na Wajumbe wengine walioongozana nao katika kuhakikisha banda lao linakuwa na bidhaa zinazo kidhi Maonyesho ya Sikuu ya Nane nane.
Habari na Picha
Ni kwa hisani ya Mtandao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni