Mtoto Wa Jinsia Mbili Ya Kike Na Kiume Azaliwa Muleba Mkoani Kagera
Mtoto wa Jinsia mbili ya kike na kiume amezaliwa katika Hospitali Teule ya Rubya iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.
Kuzaliwa
kwa mtoto huyo kumethibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo,
Dkt.Geore Kasibante (pichani), ambaye alisema hali ya mtoto huyo
inaendelea vizuri na kuwa wakati wowote atapelekwa hospitali kubwa kwa
ajili ya uchunguzi ili afanyiwe upasuaji kwa vile katika hospitali hiyo
hawana madaktari bingwa wa kuweza kufanya upasuaji huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni