Kuanzia Septemba 5 Visimbuzi ( Ving'amuzi) Kuonesha channeli za ndani BURE
Serikali
imesema kuanzia septemba 5, mwaka huu visimbuzi vitaanza kuonesha
channeli zote za ndani bila kutoza gharama yoyote kwa mtazamaji.
Akiwaeleza
waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, kuhusu yaliyozungumzwa
katika kikao kati ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini,
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.
Hassan Abbasi amesema kuwa serikali imefikia uamuzi huo baada ya
visimbuzi vya AZAM, ZUKU na DSTV kutoonesha channeli za ndani, kulingana
na aina ya leseni zao.
“Ningependa
watanzania wafahamu kwamba kuanzia septemba 5 mwaka huu, visimbuzi vya
Ting, Starmedia, Continental na Digtek vitaonesha takribani channeli 34
za ndani bure, ili kutoa fursa ya kila mwananchi kuwa na haki ya
kupata taarifa” alisema Dkt. Abbasi
Aidha,
alielezea kuwa wadau hao na wamiliki wa televisheni wameonesha
kuridhishwa na hatua hiyo kwa vile Serikali imetengeneza miundombinu
itayoruhusu channeli zao kuonekana nchi nzima.
Dkt.
Abbasi, alisisitiza kuwa “nchi imeandaa mfumo, ambao unaweza
kufanyakazi bila kutegemea kampuni kutoka nje ya nchi kwa ajili ya
kuonesha channeli za ndani au matangazo, kwa hivyo wadau au wamiliki wa
vyombo vya habari wasihofu kuhusu hilo”
Kikao
kati ya Waziri Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini,
kimefanyika kwa lengo la kuwa na majadiliano ya pamoja baina serikali na
wadau hao ili kupata muafaka kuhusu kutooneshwa kwa chaneli za ndani
katika visimbuzi vilivyokiuka masharti ya leseni zao.
Aidha,
kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia James Kilaba, pamoja na wataalamu
wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni