Dstv Tanzania

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA IGUNGA AKAMATWA IKIWA NI UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU



Jeshi la polisi wilayani Igunga limemtia mbaroni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Igunga ndugu Peter Onesmo kama ilivyoamriwa na Waziri Mkuu Mh. Kasimu Majaliwa wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Tabora.
 

Peter Onesmo na wenzake wanatuhumiwa kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha za mashine ya kukobolea mpunga Zaidi ya milioni 30 na upotevu wa fedha za mrabaha zilizokusanywa kutokana na makinikia karibia Shilingi milioni 141 mali ya kijiji cha   Bulangamilwa.

Agizo hilo la Waziri Mkuu lilitokana na kilio cha wananchi kupitia Mbunge wa Jimbo la Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali.
Akielezea kero za Wananchi wa Jimbo hilo, Mh. Seif Gulamali alimweleza waziri mkuu kuwa pamoja na upotevu huo wa fedha bado mtendaji wa kijiji alihamishwa toka kijijini cha Bulangamilwa na kupandishwa kuwa mtendaji wa kata ya Igurubi.  
 

Pia jeshi la polisi linamshikilia aliyekuwa mtendaji wa kijiji Bulagamilwa, Ntemi James kwa kuwa ndiye anatajwa kama mtuhumiwa wa kwanza katika sekeseke hilo la upotevu wa fedha sh. Milion 141 za kijiji hicho.

Watuhumiwa wote wanatarajiwa kupandishwa kizimbani pindi upelelezi utakapokamilika.

Hakuna maoni: