Dstv Tanzania

UVCCM W-NJOMBE WACHANGIA DAMU UNIT 17 NA KUFANYA USAFI HOSPITAL YA MAKAMBAKO SIKU YA MAADHIMISHO YA VIJANA DUNIAN.

Na.Titho Stambuli.

UVCCM wilaya ya Njombe wameadhimisha siku ya Vijan Duniani kwa kufanya shughuli ya kijamii kwa kufanya usafi hospital ya Makambako, kuchangia damu Unit17 na baadaye kufanya kingamano la vijana ndani ya Mji mdogo wa makambako.

Jumuiya hyo inayoongozwa na uratibu wa maswala ya kiutendaji na ndugu Daniel muhaza ambaye ameonekana kuitendea vyema nafasi yake kwa kuongoza vyema vijana wake kwa kuwa na ukomavu Wa kisiasa na kushiriki shughuli za kijamii kila siku. 


Siku ya maadhimisho ya vijana Dunian katibu aliwaongoza vijana wake kutoa huduma ya kijamii kwa kuwa ni wajibu wao kuhakikisha wanaisaidia watanzania wenzano wenye matatizo na afya lkn pia kufanya usafi ni kwa maslahi yetu sote kwakuwa hata sisi tutarudi kutibiwa hapa ama ndugu, rafiki na jamaa..


Licha ya kufanya shughuli hyo ya kijamii walifanya kongamano la vijana kuweza kukumbushana wajibu wao, kuimarisha umoja huo, na kuhakikisha vijana wananufaika na sera ya serikali ya kuwainua vijana na kuwakumbusha namna gani wanaweza kuhakikisha wanalinda Afya zao. 


Kongamano hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa mbunge wa jimbo la Makambako Mh Deo Sanga amewataka vijana kutobweteka wachape kazi ili kupata mafanikio Serikali iko kwaajili yao na wao waonyeshe juhudi zao, wasibweteke na kauli za wanasiasa wenye lengo la kuwagombanisha na Serikali,hakuna muujiza wa maendeleo zaidi ya kufanya kazi na kutambua fursa zinazo kuzunguka. 

"taifa lolote ili liendelee linahitaji nguvu kazi ya vijana wenye nidhamu, weledi na bidii ya kazi "

Akizungumza na mtandao huu katibu wa Uvccm wilaya ya Njombe siri ya kufanikiwa yote haya ni umoja, mshikamano na nidhamu ya hali ya juu kwa vijana ambao amekuwa nao katika maisha ya kisiasa kila siku na pia amesifu baadhi ya vijana wilayan Njombe kuwa wamekuwa wakijitokeza kwenye shughuli ya kijamii bila kujali itikadi za kisiasa kwa hilo tunajivunia kwa kuwaunganisha vijana wetu na pia wengi wameonyesha mapenzi ya dhati kwa Serikali ya ccm na kuunga mkono jitihada za Serikali ya CCM.

Mtandao huu unawapongeza kwa huduma ya kijamii mwenyezi Mungu awabariki

Hakuna maoni: