Dstv Tanzania

KATIBU WA UVCCM WILAYA YA UBUNGO, LEAH D. MBEKE AHITIMISHA ZIARA YA KIUTENDAJI MATAWINI, KATA YA SARANGA.

Leo tarehe 19/08/2018  katibu wa Umoja wa vijana CCM , ndugu: Leah D. Mbeke amehitimisha ziara kwa kutembelea matawi(8) ya kata ya Saranga na kukamalisha idadi ya matawi yote 16 yaliyotembelewa katika kata hiyo kuanzia siku ya jana.

Katibu amepokelewa na  Katibu wa UVCCM  kata ndugu: Enock Haule na mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM kata ndugu: Frank Michael.

Katibu anapita kukagua utendaji wa matawini kuanzia ufanyikaji wa vikao, mikutano ya wanachama wote, mawazo ya miradi, utunzaji wa kumbukumbu n.k

" Vijana msigeuze utaratibu, jifunze kuwa mnafata taratibu..kila Jambo mnalofanya hakikisheni mnatoa taarifa kwa Chama tena kwa barua..zinaitwa nakala..wapeni makatibu wenu wa tawi ambao ni walezi nakala za barua na taarifa zenu!kuacha kufanya hivyo na kufanya mambo kimyakimya ni dharau na hili ndio linasababisha kutokuwa na mshikamano, Sasa hi ifike Mwisho..kuanzia Sasa fateni utaratibu huo." alisema katibu Leah

"Msikubali kuingizwa kwenye makundi ya uchaguzi, kuweni vijana wazalendo wa kwelikweli..nikisikia kiongozi wa vijana au kijana flani anajihusisha na makundi tutaonana wabaya maana sitaunga mkono tabia zinazoigawa jumuiya yetu hata kidogo." alisisitiza katibu huyo

"Kawaambieni watu waliohaidi vijana hawa wanapokuwa wanapitapita huku matawini watekeleze ahadi zao, kama hawawezi kutekeleza basi warudi kuja kuwaambia vijana wameshindwa kutekeleza waombe radhi! Kuliko kukaa kimya au kutopokea simu za vijana, hii inaleta migogoro Kati ya wanachama hawa na viongozi wao wa tawi!na wasipofanya hivyo basi majina yao tutayapeleka sehemu husika sababu wanatuharibia jumuiya." alimalizia katibu huyo kwa msisitizo.


Matawi yaliyotembelewa siku ya leo ni Ukombozi, Stop over mama, Stop over Imara, King'ongo, Mpakani, Saranga na Tanesco.

Mpaka Sasa yametembelewa matawi 131 Kati ya matawi 137, Kata 13 Kati ya kata 14 za wilaya ya Ubungo.

Imetolewa na:
TAUSI H. RASHID
KATIBU WA HAMASA
WILAYA YA UBUNGO
DAR ES SALAAM.

#TukutaneKazini

Hakuna maoni: