MBUNGE WA JIMBO LA MAKAMBAKO AFANYA ZIARA YA KIKAZI JIMBONI KWAKE ,AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO.
Na.Titho Stambuli.
Mh Deo Sanga(JAHPEOPLE) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo La Makambako ,amefanya ziara ya kikazi jimboni kwake Makambako.
Mbunge wa jimbo hilo amefanya ziara hiyo ili kuona hali halisi ya utekelezaji wa ilan ya CCM, na kusikiliza kero zinazowasumbua wananchi ili aweze kuzisemea bungeni ziweze kutatuliwa na kero ndogondogo ofisi yake kwa kushirikiana na halmashauri ziweze kutatuliwa na pia kuimarisha mahusiano mazuri kwa wapiga kura wake.
Ziara hiyo ambayo imewashirikisha viongozi wa ccm ngazi za kata na matawi huku ngazi ya wilaya ikiwakilishwa na katibu wa vijana wa wilaya ya Njombe Ndg Daniel Muhaza.
Mheshimiwa Deo Sanga ameweza kuwahutubia wananchi waliokuwa na kiu ya kumsikia mbunge huyo ambaye ni mtu wa watu, kipenzi cha watu, amewaambia maendeleo ni mchakato na mahitaji yanabadilika kila siku hivyo Serikali inahitaji ushirikiano kutoka makundi mbalimbali ili kuweza kubaini kila aina ya changamoto na kuleta maendeleo.
"pasipo ushirikiano Hakuna jambo lolote ambalo litakwenda ,lakini pia vyama vya siasa vitumike kubaini changamoto zinazo wakabili wananchi na sio kujakuwachonganisha wananchi na Serikali, amewataka wananchi kuwapuuza wanasiasa wa namna hiyo"
Amewapongeza pia kwa kuendelea kukiamn chama cha mapinduzi kwa kuwa kimezd kuwa mkombozi wa wananchi kila siku, Serikali imezd kusogeza huduma za Afya kwa wananchi karibu ,elimu bure, miundombinu inazid kuimarishwa kila siku, maji, migogoro ya ardhi na utumishi bora, hivyo Serikali ya CCM ipo kazini na haina muda wa kuwavumilia wazembe ambao hawakotayar kuwatumikia wananchi.
Amewataka pia wananchi kumshukuru Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John pombe Magufuli kwa namna ambavyo amekuwa na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi ambao walimuamin na kumpigia kura.
Nao wananchi wa jimbo hilo wameonekana kufurahishwa na kumpongeza mbunge wa jimbo hilo kwa kufanya ziara kwa kuwa amefika kuwasikiliza wananchi wake kujua changamoto zinazo wakabili, kwao ni neema kuonana na muwakilishi wao kwa kuwa wanaamn ndio mwarobaini wao katika kupambana na maendeleo.
Wananchi hao wameweza pia kumtunuku zawadi mbunge huyo hii ni tabia njema ya mbena Mgeni akifika hawezi kukosa cha kuondoka nacho.........
Sisi tutaendelea kukuletea Habar kila siku ziara hii bado inaendelea mwakilishi wa mtandao huu Ndugu Daniel Muhaza, tunamtakia majukumu mema kwenye ziara aendelee kutuletea habar za ziara hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni