UMOJA WA"MARAFIKI WA MWALIM NYERERE”WAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI
Katika kikao cha awali cha Umoja wa"MARAFIKI WA MWALIM
NYERERE" kilichofanyika August 18/2018 katika hoteli ya Rose Garden huko
Mikocheni jijini Dar-es-Salaam kimemchagua ndugu Rashid Muhamed Rashid ( wa kwanza kushoto pichani) kutoka Zanzibar kua Makamo
Mwenyekiti wa Umoja huo.
Rashid Muhamed Rashid ambaye pia ni Mjumbe kutoka Mtandao wa
SAFARI YA CCM -2020 ameshika nafasi hiyo kuanzia August 18/2018.
Katika kikao hicho pia kimemchagua ndugu Salum Humoud Salum
kutoka Zanzibar ( wa pili kushoto) kua
Naibu Katibu wa Umoja huo wa " MARAFIKI WA MWALIM NYERERE ".Salum
Humoud Salum ambaye pia ni Katibu kutoka Mtandao wa SAFARI YA CCM-2020 ameshika
nafasi hiyo kuanzia August 18;2018.
Wengine pichani ambapo wa kwanza kutoka kulia ni Katibu wa
siasa na uenezi Tawi la CCM Bokorani ,Kata ya Mtoni ,Wilaya ya Temeke Mkoa wa
Dar-Es-Salaam ndugu Geoffrey Hinjuson ( Mkuu wa Itifaki ) na wa pili kutoka
kulia ni Mjukuu wa Hayati baba wa Taifa ;ndugu Magori John Nyerere ( Sophia
Nyerere ).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni