Mwita Waitara Ajitabiria Kushinda Tena Jimbo la Ukonga
Aliyekuwa mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara amesema kwa hali ilivyo ya kisiasa katika jimbo hilo tayari ameshinda.
Waitara
anasema anajiandaa kuendelea kuwatumikia wana Ukonga baada ya uchaguzi
wa Septemba 16, 2018 kumshinda mgombea wa Chadema, Asia Msangi.
“Mimi
ni mbunge ninayeendelea na ninapozungumza na wananchi nasema ninafanya
lakini mgombea mwenzangu wa Chadema (Asia Msangi) anasema nitafanya,
sasa huoni nimekwisha shinda,” Waitara amelieleza gazeti la Mwananchi.
Amesema
kampeni zake atazizindua rasmi Septemba mosi na kwa sasa anafanya
mikutano ya chini kwa chini kwa kukutana na makundi mbalimbali
kuzungumza nayo.
Waitara
aliyewahi kuwa CCM akahamia Chadema na kurudio tena CCM Julai 28,
ameanika mbinu zake sita zitakazomwezesha kumshinda Asia.
Amezitaja
mbinu hizo kuwa ni mikutano ya hadhara; kukutana na makundi mbalimbali
kama bodaboda; wafanyabiashara; vikoba na kutembea mtaa kwa mtaa.
“Mbinu
ya nne ni kutoa mrejesho wa miradi niliyoifanya, tano; kuonyesha kero
zilizopo na mwisho namna tutakavyozishughulikia,” amesema Waitara
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni