UGANDA WAFALME WA SOKA YA VIJANA CECAFA, WAUNGANA NA SERENGETI BOYS AFCON U17 DAR 2019
UGANDA
wameendelea kudhihirisha ubora wao katika soka ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati, baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kufuzu Fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa
ukanda wa Afrika Mashariki (CECAFA AFCON Qualifier 2019) kufuatia
ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ethiopia leo Uwanja wa Taifa wa Dar es
Salaam.
Ushindi
huo umetokana na mabao ya Kasozi Samson dakika ya 14 na Abdulwahid
Iddi, mawili dakika za 61 na 85 wakati la Ethiopia limefungwa na
Mintesnot Wakigira dakika ya 90 na ushei na sasa The Kobs wataiwakilisha
CECAFA kwenye AFCON U17 Mei mwakani hapa hapa Dar es Salaam.
Rais
wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad aliwakabidhi Kombe la ubingwa
wa michuano hiyo mipya Uganda mbele ya mamia ya mashabiki waliojitokeza
Uwanja wa Taifa.
Mapema
katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, Tanzania
walishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Rwanda baada ya sare ya 2-2.
Tanzania wamefuzu moja kwa moja kushiriki AFCON U17 Mei mwakani kwa sababu wao ndio wenyeji wa michuano hiyo.
Ethiopia
imetoa Kipa Bora wa Mashindano Alazar Mako na mfungaji bora, Mintesnot
Endrias Wakijira aliyefunga mabao nane, wakati Mchezaji Bora ni Kelvin
Pius John wa Tanzania iliyotwaa pia tuzo ya Mchezo wa Kiungwana.
Timu
nyingine zilizoshiriki michuano hiyo iliyoanza Agosti 11, mwaka huu ni
Burundi, Djibouti, Kenya, Somalia, Sudan Kusini na Sudan.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni