YANGA SC KUIFUATA RAYON BILA MAKAPU, AMEFIWA NA MAMA YAKE MZAZI MAZISHI LEO ZANZIBAR
KIUNGO
wa Yanga SC, Said Juma ‘Makapu’ hatasafiri na timu kwenda Kigali nchini
Rwanda kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho
Afrika dhidi ya Rayon Sport, kufuatia kufiwa na mama yake mzazi nyumbani
kwao Zanzibar.
Taarifa
ya Yanga SC jana imesema kwamba mama yake Makapu amefariki dunia jana
asubuhi huko Bububu visiwani Zanzibar na mazishi yanatarajiwa kufanyika
leo baada ya sala ya Adhuhuri.
Kikosi
cha Yanga kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam leo usiku kwenda Kigali
kwa ajili ya mchezo huo wa mwisho baada ya kushinda mechi moja tu kati
ya tano za awali, kufungwa tatu na sare moja.
Mchezo huo utakaofanyika Jumatano kuanzia Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Nyamirambo, utachezeshwa na marefa kutoka Uganda, Mashood Ssali atakayepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera Mark Ssonko na Dick Okello.
Mchezo
wa kwanza baina ya Yanga na Rayon Sport, wote mabingwa wa zamani wa
Afrika Mashariki na Kati timu hizo zilimaliza kwa sare ya 0-0 Mei 16
Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Yanga
SC inashika mkia katika kundi D, ikiwa na pointi nne tu, nyuma ya Rayon
yenye pointi sita, wakati Gor Mahia na USM Alger kila moja ina pointi
nane na zinamenyana kwenye mechi ya mwisho Jumatano pia mjini Algiers.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni