SAMATTA AENDELEZA MOTO WA MABAO KRC GENK IKIPIGA MTU MABAO 3-2 LIGI YA UBELGIJI
NAHODHA
wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi na kuifungia timu
yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Waasland
Beveren katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa
Luminus Arena.
Samatta
aliingia uwanjani dakika ya 58 kuchukua nafasi ya mshambuliaji
Mbelgiji, Zinho Gano na ikamchukua dakika 20 tu kuifungia bao Genk
akimalizia pasi ya kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy.
Kabla
ya kutoka, Gano alimsetia mshambuliaji Mkosovo mzaliwa wa Ujerumani,
Edon Zhegrova kuifungia Genk bao la kwanza dakika ya 20 na bao lingine
la timu hiyo limefungwa na mshambuliaji mwingine Mbelgiji, Leandro
Trossard dakika ya 89.
Mabao
yote ya Waasland Beveren yamefungwa na kiungo Mghana, Nana Opoku
Ampomah dakika za 66 na 75 na kwa matokeo hayo sasa Genk inapanda
kileleni, ikifikisha pointi 13 baada ya mechi tano, ikiwa mbele ya Club
Brugge yenye pointi 13 pia, Anderlecht pointi 12 na Standard Liege
pointi 11 baada y azote kucheza mechi tano tano pia.
Kikosi
cha KRC Genk: Vukovic, Nastic, Dewaest, Aidoo, Maehle,
Heynen/Malinovskyi dk74, Seck, Pozuelo, Paintsil, Zhegrova/Trossard dk67
na Gano/Samatta dk58.
Waasland
Beveren: Roef, Massop, Boljevic, Forte/Ndao dk45, Jubitana/Van Damme
dk76, Keita, Ampomah, Caufriez, Abdullah/Badibanga dk63, Vukotic na
Schryvers.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni