BARAZA KUU LA KIKANUNI UVCCM WILAYA YA UBUNGO LAMALIZIKA SAA SITA NA ROBO USIKU.
Siku ya tarehe 26/08/2018 (Jana) kumefanyika baraza kuu la UVCCM wilaya ya Ubungo la kikanuni ikiwa na baraza la kwanza kwa Mwaka 2018 la kikanuni chini ya Mwenyekiti wake ndugu: EDWIN C. MREMA, Katibu ndugu: LEAH D. MBEKE, Mhamasishaji ndugu: TAUSI HASSAN, Wajumbe wa kamati ya utekelezaji, ndugu : TIJA MAGOMA, Ndugu: SAID MASSOD na YUSUPH RAMADHAN.
Kikao hiki ni kikao kikubwa katika jumuiya hii na hufanyika mara 2 kwa Mwaka kwa mujibu wa kanuni, kimefanyika GOLDEN PARK, SINZA.
Baraza hili lilifunguliwa na MNEC wa Mkoa wa Dar es salaam na mjumbe wa kamati ya Siasa na maadili ndugu: ISSA MTEMVU na kufungwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo ndugu: LUCAS MGONJA aliyeambatana na Kamati yake yote ya Siasa wilaya ya Ubungo.
Katiba baraza hili wajumbe walitumia muda wao bila kujali kuwa ni usiku kujadili kikamilifu mustakabali wa vijana wa Ubungo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ili kuhakikisha malengo ya vijana wa Ubungo yanatimia.
Umoja Wa Vijana wa CCM wilaya ya Ubungo, umejipanga kikamilifu kupambana na wale wote watakaoonesha nia ya kukwamisha juhudi za Rais Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI katika kuleta maendeleo.
Baraza limetuma salamu kwa wafuatao
1. Baraza limetuma salamu kwa viongozi wote wa kiserikali (wachaguliwa) ndani ya wilaya ya Ubungo wanaosahau Vijana wakishika nafasi hizo na kuacha kuwathamini vijana wanaotoka kwenye maeneo yao, wengine simu hawapokei kuwa endeleeni kutengana vijana na sisi tutawatenga!.
2. Baraza limetuma salamu kwa WALEZI wote wa jumuiya hiyo kuanzia ngazi ya Tawi na Kata ambao hawashiriki vikao vya vijana vya kikanuni na kuwaelekeza na kuwa sehemu ya kuzorotesha jumuiya kuwa hawatafumbiwa macho tena, ambaye hatakuwa anashiriki vikao na kuwaelekeza vijana basi vikao vitakaa na kuazimia!.
3. Viongozi wa kata ambao hawafanyi kazi zao kikamilifu na kwa kulegalega wamepewa muda wa kujitathmini kwani kasi ya utendaji kazi tunayoenda nayo haihitaji watu wavivu.
4. Viongozi wote waliowahaidi vijana kwenye matawi na kata wahakikishe wametekeleza ahadi zao.
Pamoja na hayo, baraza lilimpokea rasmi mjumbe wa baraza hilo ndugu: TIJA MAGOMA ambaye ni katibu mpya wa CCM wilaya ya Ubungo, ndugu: Tija alikesha na vijana katika baraza hilo na kushiriki kikamilifu ajenda zote.
#UBUNGOTUKOKAZINI
#TUNALINDACHAMANASERIKALI
Imetolewa na:
TAUSI HASSAN
KATIBU WA UHAMASISHAJI
WILAYA YA UBUNGO
DAR ES SALAAM

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni