PICHA: Rais Uhuru Kenyatta Alivyokutana na Trump Ikulu ya Marekani
Rais
Donald Trump wa Marekani amekutana na mwezake wa Kenya Uhuru Kenyatta
mjini Washington na kuzungumzia masuala mbalimbali, zaidi wakiangazia
biashara na usalama.
Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya Marekani, wakati wa ziara hiyo mataifa hayo mawili yalikubaliana na kutangaza mikataba ya jumla ya $900 milioni.
Rais
Kenyatta ni kiongozi wa tatu kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara
kukaribishwa Ikulu ya White House na kufanya mazungumzo na Rais Trump.
"Tumekuwa
na ushirikiano mzuri na wa kipekee na Marekani katika masuala ya
usalama na ulinzi, hasa katika harakati za kukabiliana na ugaidi. Muhimu
zaidi tuko hapa kuboresha ufungamano wetu katika biashara na uekezaji, "
kasema Rais Kenyatta.
Rais Trump alisema Kenya na Marekani zitaendelea kushirikiana kuimarisha ufungamano wao katika biashara, uekezaji na usalama.
"Tunafanya
shughuli nyingi za utalii, biashara na ulinzi. Na kwa wakati huu
tunajibidiisha kuboresha usalama," alisema Rais Trump. " Tunafurahia
sana kuwa nawe hapa."
Miongoni
mwa mengine, Bw Trump alifurahia pendekezo lililowasilishwa na kampuni
ya ujenzi kutoka Marekani Bechtel Corporation kutaka kupewa kandarasi ya
ujenzi wa barabara ya kisasa ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa.
Mataifa yote mawili yalikubaliana na kuendelea na mashauriano zaidi ili kuafikiana kuhusu ufadhili wa ujenzi huo.
Viongozi
hao wawili walijadiliana pia kuhusu safari za ndege za moja kwa moja
kutoka Nairobi hadi New York zitakazoanza mwezi Oktoba mwaka huu na
kukubaliana kwamba safari hizo za ndege zitaimarisha zaidi utalii na
biashara kwa manufaa ya nchi hizi mbili.
Marekani
ndiyo chanzo kikuu cha watalii wanaozuru Kenya na taifa hilo la Afrika
Mashariki linatarajia kutumia fursa ya safari za moja kwa moja za ndege
za Kenya Airways kati ya mataifa hayo mawili ambazo zitaanza Oktoba 28
kuimarisha idadi ya watalii wanaofika kenya.
Viongozi
hao wawili kwa pamoja wamejadili njia za pamoja za kupambana na ugaidi
na ushirikiano wa kibiashara. Mpango wa upanuzi wa barabara inayohusisha
miji mikubwa ya Kenya, Mombasa na Nairobi pia ilijadiliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni