Sababu 2 za Jackline Wolper kutoswa shindano la Miss Tanzania
Hatimaye
imebanika sababu ya Jackiline kutoswa kwenye kamati ya Majaji ya Miss
Tanzania kwenye fainali ya mashindano yaliyofanyika Kanda ya Ziwa hivi
karibuni.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo August 27, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni
ya The Look inayosimamia Mashindano hayo, Basilla Mwanukuzi ameleza
sababu za Wolper kutolewa.
"Katika
ngazi ya kanda Majaji ni kamati ya Miss Tanzania au watu ambao kamati
itapendekeza, sasa Wolper sio kamati ya Miss Tanzania," amesema.
"Lakini
pia Majaji wanapewa semina, Wolper alichelewa kufika kwenye semina,
ataingiaje kujaji hajaongozwa?. Sio tu uwe super star uje kujaji,
hapana! kuna miongozo maalumu alitakiwa awahi ahudhurie semina ambayo
wale Majaji wengine walipewa, yeye kafika semina imeshaisha," amesema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni