CAF yaridhishwa na maandalizi ya AFCON
RAIS
wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Ahamd Ahmadamesema
ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 (AFCON).
Mashindano
ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 AFCON
yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.
Ameyasema
hayo jana (Jumatatu, Agosti 27, 2018) wakati akizungumza Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
Pia
ameihakikishia Serikali kwamba hakuna mabadiliyo yoyote ya ratiba
yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.
Rais
wa CAF yupo nchini kwa ajili ya kuongoza mkutano maalum wa mabadiliko
ya katiba ya Baraza la Vyama vya Soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati (CECAFA).
Mkutano
huo unaofanyika jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa na viongozi wa juu
wa nchi wanachama wote 12 wa CECAFA wakiwemo marais.
Kwa
upande wake,Waziri Mkuu WAZIRI amesema mechi zoteza michuano ya Afrika
ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON) zitafanyika jijini Dar es
Salaam.mashindano
“Tupo
katika hatua za mwisho za maandalijzi ya michuano hiyo itakayofanyika
jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Taifa, Uhuru, Chamanzi na JK
Park utatumika kwa mazoezi.”
Waziri
Mkuu amesema ni muhimu kwa nchi kushiriki katika mashindano makubwa
kama hayo kwa kuwa yanasaidia kwenye ukuzaji wa vipaji kwa vijana ambao
wengi wao ni wanafunzi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, AGOSTI 27, 2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni