Serikali yathibitisha kuwepo kwa saruji ya kutosha nchini........Wanaopandisha Bei Kiholela Kunyang’anywa Leseni
Serikali
imethibitisha kuna saruji ya kutosha nchini baada ya kuwepo kwa hifadhi
ya Tani 16,000 kwa jana pekee ambapo uzalishaji ukiendelea vizuri
utafikia Tani Milioni 5.8 kwa mwaka wakati mahitaji ya mwaka ni tani
Milioni 4.8.
Kutokana na hali kuwa hivyo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewaagiza watengenezaji saruji kuwafutia leseni mawakala ambao watabainika kupandisha bei huku pia akitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni kutoka nje kuja kununua saruji nchini.
Kutokana na hali kuwa hivyo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewaagiza watengenezaji saruji kuwafutia leseni mawakala ambao watabainika kupandisha bei huku pia akitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni kutoka nje kuja kununua saruji nchini.
Mwijage
ametoa kauli hiyo jana Agosti 27, 2018 jijini Dar es Salaam wakati
alipotembelea kiwanda Tanzania Portland Cement (Twiga) kilichopo Wazo
na Camel Cement Company kilichopo Mbagala.
Akizungumza
na uongozi wa kiwanda kinachozalisha saruji ya Twiga, Mwijage alisema
lazima baadhi ya mawakala watolewe kafara ili kudhibiti hali hiyo.
Pia
ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kumpatia orodha ya mawakala wote
wanaosambaza bidhaa hiyo pia waagizwe kushusha bei ya saruji ambayo
sasa imepaa hadi Sh 18,000 katika baadhi ya maeneo.
“Mimi
nimefanya kazi hapa miaka 18, nafahamu mchezo wote wa vijana wako
wanaoufanya, ndio maana nakuagiza uniletee orodha ya mawakala wote
wanaosambaza saruji ili niwabaini na kuwafutia leseni.
“Kwa
sababu sasa Dangote anazalisha tani 4,500 kutoka tani 2000 kwa siku,
Twiga anazalisha tani 6,000 kutoka tani 3,500 kwa siku, Tembo tani
1,100, Nyati tani 2,000 hivyo hakuna uhaba wa saruji sasa. Tayari hali
imetangamaa ila kwanini bei iendelee kubaki juu.
“Kiujumla
kwa siku tunazalisha tani 16,000 na sasa tunatumia tani milioni 5.8
kutoka tani milioni 4.8 kwa mwaka na viwanda vyote vilivyosimikwa sasa
vina uwezo wa kuzalisha tani milioni 10.5 kwa mwaka,” alisema.
Aidha,
alisema ili kuendelea kuhimili soko la ndani na la nje, tayari kuna
viwanda vitatu ambavyo ni cha Mamba, Nyati namba 2 na kiwanda cha
wachina cha Engian ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha malighafi
inayotumika kuzalisha saruji (clinker) zaidi ya tani milioni saba kwa
mwaka.
“Suala
hili la saruji kupanda, naomba watu wanivumilie, dawa ya kupanda
naijua, saruji imejaa sokoni, bei inashuka yenyewe, ila wale
wanaopandisha inaitwa ‘profiteering’ siku ya kiama inshallah basi hukumu
ni yao kama wanataka kuishi duniani shauri yao hukumu ni yao.
Aidha,
Meneja Undelezaji Biashara wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC),
Mhandisi Danford Semwenda ni kazi ngumu kuwadhibiti mawakala wa uuzaji
wa saruji hiyo hivyo wanaomba ushirikiano kutoka serikali ili kudhibiti
hali hiyo.
Kwa
upande wake Meneja Mkuu Msaidizi wa Kiwanda cha Camel, Ghalib Hassan
Ghalib alisema kutokuwapo kwa umeme wa uhakika nao umekuwa kikwazo kwa
kiwanda hicho kufikia malengo ya kuzalisha tani 600 kwa siku na hivyo
kuzalisha tani 400.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni