Serikali Yaweka Mikakati Thabiti Ili Kudhibiti Ugonjwa Wa EBOLA Usiingie Nchini
Na WAMJW – KAGERA, NGARA
Serikali
kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
inaendelea kuweka mikakati thabiti katika maeneo yote hatarishi ikiwemo
mipakan na njia za panya ili kudhibiti ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe Ummy Mwalimu jana wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa
Rusumo kati ya nchi ya Tanzania na Rwanda ili kuangalia ni jinsi gani
Mkoa wa Kagera umejipanga katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola
kuingia nchini.
Waziri
Ummy amesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umetokea eneo la
Kivu katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo unaiweka Tanzania katika
hatari zaidi ya kuweza kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na muingiliano
wa wananchi baina ya nchi hizo.
“Mlipuko
huo wa Ugonjwa wa Ebola ambao umetokea katika Jamhuri ya Demokrasia ya
Kongo sasa hivi inatuweka Tanzania katika hatari kubwa zaidi kupata
wagonjwa kutokana na mlipuko huo kutokea eneo la Kivu Kaskazini ambalo
ni karibu na Tanzania na muingiliano wa wananchi baina ya nchi hizi
mbili ni mkubwa ” Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha,
Waziri Ummy alisema kuwa Serikali inaendelea kutoa mafunzo kwa wahudumu
wa Sekta ya Áfya ili kufahamu jinsi ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na
Virusi vya ugonjwa wa Ebola sambamba na hilo Serikali imeleta vifaa
kinga watakavyovaa wakati wakitoa huduma kwa mgonjwa au mhisiwa wa
ugonjwa wa Ebola.
“Kama
Serikali, kubwa ambalo tumelifanya ni kuhakikisha tunatoa mafunzo kwa
watoa hudumu wa sekta ya Áfya nchini.kwa mujibu wa taarifa ya WHO nchini
Kongo watoa huduma wa Áfya 9 wamepata ugonjwa wa Ebola huku mmoja
amefariki” Alisema Waziri Ummy.
Pia
Waziri Ummy alimwagiza Mkuu wa mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatenga
Zahanati moja katika maeneo ya mipaka ambayo itakuwa inapokea wahisiwa
au wagonjwa wa Ebola, vivyo hivyo kwa ngazi ya Wilaya kutenga hospitali
kwa ajili ya wahisiwa pindi utapoingia nchini.
Hata
hivyo h Waziri Ummy amewataka wananchi wanaokaa katika vijiji vya
mipakani ambavyo vinapokea watu kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na
Burundi wamuonapo mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola wamwelekeze
kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyo jirani.
”
Wananchi ambao wanakaa mipakani hasa katika vijiji ambavyo vinapokea
watu kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na Burundi mnaowajibu wa
kuhakikisha mnafuata taratibu za uhamiaji, lakini pale ambapo mtu
ameingia na ana dalili za ugonjwa wa Ebola muelekezeni aende kwenye
vituo vya kutolea huduma za Afya” alisema Waziri Ummy
Kwa
upande mwingine Waziri Ummy alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya
Áfya imeajiri Watumishi wapya wa Sekta ya Áfya 33 ambao wamesambazwa
kwenye maeneo ya mipakani ili kusaidia kudhibiti ugonjwa wa Ebola
usiingie nchini.
“Zuli
ambalo tumelifanya, tumeajiri watumishi wapya wa Áfya 33 kwa ajili ya
kuwasambaza katika maeneo haya ya mipakani ili kudhibiti ugonjwa huu wa
Ebola usiingie nchini kwetu” alisema Waziri Ummy.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amekiagiza kitengo cha Elimu ya Áfya kwa umma
kutoka Wizara ya Áfya kutoa Elimu juu ya ugonjwa wa Ebola kwenye
Serikali za vijijini kupitia Redio, vipeperushi, video jambo
litalosaidia kuweka msukumo kwa wananchi ili kujua athari za ugonjwa huo
kwa maendeleo ya Taifa.
Mwisho Waziri Ummy aliendelea kuwatoa hofu wananchi wa Tanzania kuwa ugonjwa wa Ebola bado haujaingia nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni