Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.
Serikali
imepanga kuzalisha mitamba zaidi ya milioni 1 kwa mwaka ili kukuza
sekta ya mifugo hapa nchini ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Akizungumza
katika kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari- MAELEZO,
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema kuwa Serikali
imejipanga kuhakikisha kuwa sekta hiyo inatoa mchango mkubwa katika
ujenzi wa uchumi na ustawi wa wananchi.
“Vituo
vya uhaulishaji vilivyopo Arusha na Sao Hill Iringa vimeboreshwa ili
viweze kutoa mbegu bora za kutosha kwa kufanya maboresho makubwa katika
vituo vya kanda vya uzalishaji mbegu za mifugo” alisisitiza Mpina
Amesema
kuwa kuelekea uchumi wa viwanda, Serikali imejipanga kuzalisha mifugo
mingi ya kutosha ili kupata bidhaa bora zitokanazo na mifugo, Aliongeza
kuwa Serikali imevunja mikataba na wawekezaji wengi ambao hawakuweza
kutimiza malengo ya uwekezaji katika sekta ya mifugo.
Katika
kuboresha sekta ya uvuvi Waziri Mpina amesema wafanyabiashara watumie
fursa ya kuzalisha nyavu halali ili kuchochea ukuaji wa sekta ya uvuvi
kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya bidhaa za uvuvi.
Pia aliwaasa Viongozi wote wa Serikali kutojiusisha na uvuvi haramu kwani ni kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Katika
kuimarisha sekta ya mifugo amesema kuwa Serikali imeendelea kukusanya
madeni yanayodaiwa na NARCO ambapo zaidi ya bilioni 3 zimekusanywa.
Kipindi
cha ‘TUNATEKELEZA’ kinarushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
na kuratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO kikiwashirikisha Mawaziri wote
kwa awamu hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni