Waziri Mkuu Akwea Pipa Leo Kuelekea China Kumwakilisha Rais Magufuli
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Ijumaa, Oktoba 31, 2018)
kuelekea nchini China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi
na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Mkutano
huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini
Beijing nchini China, ambapo utafunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping.
Katika mkutano huo Waziri Mkuu anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli.
Mbali
na kuhudhuria mkutano huo pia, Waziri Mkuu anatarajia kukutana na
kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa kampuni mbalimbali akiwemo Rais
wa Kampuni ya CCECC, Rais wa Shirika la NORINCO, Rais wa Kampuni ya
Zijin Gold Mine pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya saruji ya HEGNYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni