UVCCM NJOMBE WAMLILIA DADA WA RAISI MAGUFULI.
UVCCM MKOA NJOMBE:
Sisi UVCCM Mkoa NJOMBE tunatoa Pole kwa Mh.Raisi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa msiba wa Dada yake Monica Joseph Magufuli.
Tunawaombea Mungu awape Faraja ya Pekee katika kipindi hiki kigumu kwao Ndugu jamaa na Marafiki.(Mbali na kuwa na misiba kila siku lakini Msiba ukikufika haujawahi kuzoeleka)
RIP Mama Yetu Monica Magufuli mbele wewe Nyuma tutafuata sisi tuu Mmoja baada ya Mwingine kwa kadri ya Ulivyopangiwa na Mungu.
Kwetu sisi tuliobaki kwenye Fumbo hili hatujui nani atakayefuata na lazma apatikane wakufuata hivyo kikubwa tuzidi kujiweka salama katika mikono ya Mungu kwakujitakasa Mioyo yetu na kutenda yanayompendeza Mungu.
Johnson Elly Mgimba.
Katibu H&C UVCCM-Mkoa Njombe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni