Anthony Mavunde: Uchaguzi Mdogo Unaofanyika Nchini Hauathiri Idadi Ya Viti Maalumu
Serikali imesema mabadiliko yanayotokea katika uchaguzi mdogo wa ubunge, hayaathiri idadi ya viti maalumu vya chama husika.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde
amesema hayo akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Angelina
Malembeka aliyetaka kujua hatima ya wabunge walioingia bungeni kupitia
asilia za majimbo yao ya uchaguzi.
“Kwa
kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeongeza idadi ya majimbo, je ni lini
wabunge wapya wa CCM kupitia viti maalumu wataingia bungeni?” alihoji
Malembeka.
Akijibu
swali hilo Mavunde amesema idadi ya wabunge wa Viti Maalumu kwa kila
chama inapatikana wakati wa uchaguzi mkuu ambao hufanyika kila baada ya
miaka mitano.
“Hata
hivyo, serikali imeendelea kupokea maoni na ushauri kuhusu jambo hili,
kutokana na hali ilivyo kwa sasa Katiba na Sheria za nchi vitaendelea
kuwa msingi mkuu wa ufafanuzi na mgawanyo wa wabunge wa viti maalumu
bungeni,” amesema Mavunde.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni