Darasa la saba kuanza mtihani kesho
Baraza
la Taifa la Mitihani (Necta), limetangaza rasmi kuanza kwa Mtihani wa
Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), utakaofanyika kesho Septemba 5 na 6,
2018 nchini nzima.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 4, 2018, kuhusu mtihani
huo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema jumla ya
watahiniwa 960, 202 wamesajiliwa.
Kati
ya watahiniwa hao, Dk Msonde amesema wasichana ni 503, 972 sawa na
asilimia 52.49 na wavulana ni 456,230 sawa na asilimia 47.51.
Katibu mtendaji huyo amesema watahiniwa wasioona waliosajiliwa ni 90, wasichana 31 na wavulana 59.
Wenye uoni hafifu ambao wanahitaji maandishi makubwa ni 846, wavulana 475 na wasichana 371.
Dk
Msonde amesema mtihani huo ni muhimu kwa wanafunzi kwa ajili ya kupima
uwezo na uelewa wa wanafunzi katika yale yote waliyojifunza kipindi ha
miaka saba.
"Matokeo
ya mtihani huu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na
elimu ya Sekondari, hivyo hatutasita kuchukua hatua kwa yeyote
atakayejihusisha na udanganyifu na kuharibu taratibu zilizowekwa,"
amesema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni