China Kushirikiana na Nchi za Afrika Katika Mambo Makuu Nane ( 8)
Beijing-CHINA:
RAIS wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping amesema, Serikali ya nchi
hiyo ipo tayari kushirikiana na Afrika katika maeneo makubwa nane
katika kipindi cha miaka mitatu ijayo itayojikita katika masuala ya viwanda, miundombinu, biashara, kilimo, ulinzi na usalama pamoja na mazingira.
Akifungua
Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Bara la Afrika
(FOCAC) jana Beijing China na Rais Xi Jinping ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Jukwaa hilo alisema katika masuala ya viwanda, uchumi wa Bara la
Afrika na usafirishaji wa bidhaa utaendelea kupewa kipaumbele na
Serikali ya China pamoja na makampuni yake yanahimizwa kuwekeza katika
nchi za Afrika.
Kuhusu
sekta ya kilimo, Rais Xi Jinping alisema Serikali ya China imepanga
kuanzisha miradi 50 itayogharimu kiasi cha Yuan Bilioni 1 (Dola Milioni
147) itayosaidia masuala ya dharura na majanga mbalimbali ya kibinadamu
sambamba na hilo, Rais Xi Jinping ameahidi kupeleka wataalamu 500 wa
masuala ya kilimo ili kusaidia maendeleo ya sekta hiyo Barani Afrika.
Akizungumzia
kuhusu masuala ya miundombinu, Rais Xi Jinping amesema Serikali ya
China itafanya juhudi na Umoja wa Afrika kuunda mpango wa ushirikiano wa
Miundombinu baina ya Bara la Afrika na China na kusaidia makampuni ya
Serikali ya China kupata fursa ya ujenzi wa miradi mbalimbali.
Katika
masuala ya Biashara, Rais Xi Jinping alisema China itaongeza uingizaji
wa bidhaa zinazotoka nchi za Afrika ili kuweza kuzisaidia kukuza
biashara za kimataifa na kuahidi kupunguza kodi mbalimbali za bidhaa
kutoka Bara la Afrika.
Aidha
Rais Xi Jinping alisema katika eneo la uhifadhi na ulinzi wa Mazingira,
Serikali ya China imepanga kuanzisha miradi 50 itayosaidia mfumo wa
bioanuai na ulinzi wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi na kulinda uifadhi wa wanyama pori.
Akifafanua
Zaidi, Rais Xi Jinping alisema China pia imekusudia kuwajengea uwezo
vijana wa Bara la Afrika katika mafunzo ya ufundi stadi ambapo imepanga
kutoa nafasi 1000 katika hadhi ya juu, nafasi za ufadhili wa masomo
50,000 pamoja na kuwakaribisha vijana 2000 kutembelea masuala
mbalimbali.
Katika
eneo la afya, Rais Xi Jinping alisema Serikali ya China imepanga
kuendeleza miradi 50 katika sekta ya afya, hususani vituo vinavyolenga
kupunguza magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi, kifua na malaria.
Kuhusu
mahusiano ya mtu mmoja mmoja Rais Xi Jinping alisema Serikali ya China
imepanga kuanzisha taasisi ya mafunzo kwa watu wa Bara la Afrika na
kubadilishana fikra na mitazamo.
Aidha
Rais Xi Jinping alisema katika Nyanja ya Amani na Usalama, China
itaendelea kuweka mfuko maalum wa fedha na kusaidia Jeshi la Umoja wa
Afrika ikiwemo kuanzisha miradi 50 ya kusaidia katika masuala ya kulinda
amani, kupambana na uharamia na ugaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni