Dstv Tanzania

Majaliwa Akutana Na Waziri Wa Kilimo Wa China

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Changfu wakati alipotembelea Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo iliyopo Beijing Septemba 3, 2018.  Majaliwa yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya Afrika na China – FOCAC
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo wa China, Bw.  Han Changfu (kushoto) wakati alipotembelea Wizara hiyo iliyopo Beijing, Septemba 3, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Chanfu  wakishuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya Uvuvi kati ya China na Tanzania kwenye ukumbi wa Wizara ya Kilimo ya China katika jiji la  Beijing, Septemba 3, 2018. Wanaotia Saini ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na  Uvuvi wa Zanzibar, Rashid Ali Juma (kushoto) na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Qu Dongyu

Hakuna maoni: