KATIBU MWENEZI CCM MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE AWASILISHA KILIO CHAKE MBELE YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO JUU YA UKIRITIMBA UNAOFANYWA NA WAFANYABIASHARA WA PEMBEJEO ZA KILIMO NA WALANGUZI WA MAZAO,AWASHUTUMU MAAFISA KILIMO KWA KUTOWATEMBELEA WAKULIMA.
Na.Erasto Mgeni.Njombe.
Naibu waziri wa Kilimo na Mifugo Mh.Omary Mgumba katika
ziara yake leo amewatem,belea Viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe kwa lengo la
Kusalimiana pamoja na kupata Taarifa Fupi ya utekelezaji na usimamizi wa ilani
ya CCM Katika Shughuli mbalimbali za Maeneleo Ikiwemo Sekta Mtambuka ya Kilimo.
Naibu Waziri Mgumba amewatembelea Viongozi hao katika Ogisi
za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Humo zilizopo katika Kata na Mtaa wa Mji Mwema
Mjini Njombe Huku akipongeza uongozi wa Chama
Chama Hicho Kwa kufanikiwa Kuendelea na Ujenzi
wa Ofisi za Chama hicho ambao mpaka sasa
umefikia zaidi ya asilimia 75.
“Siwezi kuja kuongea na wadau wa sekta ya kilimo bila
kupitia katika ofisi za chama kilichoniweka madarakani”
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Mh Omary Mgumba mapema leo |
Mara baada ya Kupokea Salamu za Chama kutoka kwa Katibu wa
CCM Mkoa wa Njombe Ndg.Hosea Mpagike ambaye amemshukuru naibu waziri kwa uamuzi
wake wa kukitembelea chama hicho ambacho ndio kimemuweka madarakani tofauti na
baadhi ya viongozi wengine wa serikali wakiwemo mawaziri ambao huwa wanapita
bila kuwajulia hali ili hali chama hicho ndio kimewaweka madarakani.
Wakwanza Kushoto ni Naibu waziri wa Kilimo Mh.Omary Mgumba akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Hosea Mpagike. |
Hata Hivyo Hosea Mpagike alimpa Nafasi Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Maarufu kwa Jina la Shikamoo
Parachichi Ndugu Erasto Ngole ambaye baada ya Kupata Nafasi Hiyo Bwana Ngole
alielekeza Kilio chake kwa Naibu waziri Juu ya Wafanyabiashara wa Pembejeo za
Kilimo Ikiwemo Mbolea huku akibainisha
kuwa wapo wafanyabiashara mkoani humo wanaouza mbolea kwa bei ya juu tofauti na maelekezo ya serikali.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe ambaye pia ni Diwani wa Viti maalumu Angela Mwangeni akipiga Makofi kuashiria amefurahia moja ya Jambo lililozungumzwa na Katibu Mwenezi Erasto Ngole. |
Bwana Ngole akiongoea kwa Machungu Mbele ya Nasibu Waziri
amehoji kutokana na Hali hiyo Je Hakuna mamlaka ambazo zinasimamia? Huku akisema
kuwa wakulima wanalizwa sana na wafanyabiashara Mamluki wanaojipandishia Bei
Kiholela.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti naye alipata Fursa ya Kuzungumza na Naibu waziri wa Kilimo. |
“Mh Naibu Waziri Ukisimama Sahizi ukaenda kijijini kwangu
ambako ni kilomita Karibu 1O kutoka katikati
ya mji utakwenda kuwakuta
wafanyabaishara wanaouza mbolea wote wako kwenye Center moja, lakini unakuta mfano mbolea ya DAP Center moja
mwingine anauza elfu 58,mwingine elfu 56,mwingine anauza elfu 55
mfuko huohuo wa DAP,sasa unajiuliza hakuna mamlaka zinazosimamia?” amesema
Ngole Nakuongeza “Kila mmoja akiamka anapanga Beikama anavyotaka nasema hivi
kwasababu juzi nimenunua Mbolea,sasa haya yanafanyika Ndani ya Mji je nje ya
mji itakuwaje?
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akisalimia na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti alipowasili katika Ofisi za CCM Mji mwema |
Katika Hatua Nyingine
Bwana Ngole Ameelekeza Kilio chake kwa Naibu waziri juu ya Tatizo la wataalamu kutowafikia
Wakulima katika maeneo yao.
Amesema wakulima bado wanalima kilimo cha Mazoea licha ya
kuwa na wataalamu wachache lakini amesema haiwezekani mkulima asikutane na
mtaalamu kwa zaidi ya miaka Miwili.
“Ni kweli watanzania ni wengi na nchi ni kubwa na wataalamu
ni wachache lakini siamini kama uchache wa wataalamu unaweza ukamfanya mkulima
asikutane na mtaalamu hata kwa miaka miwili”amesema Ngole.
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akisalimia na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe Angela Mwangeni. |
Kuhusu Tatizo la Lumbesa amesema imefika wakati
wafanyabiashara wa zao la Viazi wamekuja na njia Nyingine ya kuwaibia
wakulima,kwani sasa ule ujazo wa Kilo100 kwa gunia haupo tena ila wafanyabiashara
hao wanafungasha kwa ujazo wa kilo 75 huku wakinunua kwa bei ya Chini.
"Sasa badala ya kujaza kiroba cha kilo 100 wameikata ile
lombesa lile gunia kubwa wamelikata mara tatu kwahiyo wanafunga kilo 75,75,75
inahesabika ni gunia 1"
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akisalimia na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Njombe Daniel Mahanza |
Kwa upande wake Naibu waziri Kilimo Omary Mgumba akijibu malalamiko hayo amekiri
kuwepo kwa upungufu wa Maafisa Ugani huku akiwataka waafisa ugani waliopo wafanye
kazi kwa kusaidiana na viongozi wengine ili kuwa karibu na wananchi huku
akiahidi kuendelea kulisimamia swala hilo.
Amesema Serikali inaendelea Kutekeleza Mikakati mbalimbali
kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanafikiwa na hudumu zote Muhimu hususani
katika sekta ya Kilimo.
Wa Kwanza ni Erasto Ngole Katibu Mwenezi Mkoa wa Njombe,Mh.Omary Mgumba Naibu waziri wa Kilimo na Hosea Mpagike katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Wakiwa katika Ukumbi wa mikutano unaoendelea Kujengwa. |
Hapa Chini Nimekuwekea Picha Zote Kuanzia Mapokezi ya Nje,Ndani mapaka wakati akikagua Ukumbi wa Mikutano wa CCM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni