KATIBU MWENEZI WA CCM MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE (SHIKAMOOPARACHICHI)AWAKUTANISHA WANDISHI WA HABARI WA MKOA WA NJOMBE HUKU AKISHIRIKI NAO CHAKULA CHA MCHANA………AJIVUNIA MAMBO MAKUBWA YANAYOFANYWA NA SERIKALI YA CCM CHINI YA RAISI DKT. JOHN MAGUFULI KATIKA MKOA WA NJOMBE.
Katika kuhakikisha chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Kinaendelea
kuwa karibu na wananchi kupitia kwa waandishi wa Habari Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa Chama hicho Erasto Ngole(SHIKAMOOPARACHICHI) amelazimika kukutana na wandishi wa Habari na kuwandalia Tafrija Fupi kwa kushirikia nao
Chakula cha Mchana wa Leo Tar 06/09/2018.
Katika Tafrija Hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Kimataifa yenye Hadhi ya Nyota 3 Hillside Hotel imelenga kudumisha mahusiano mema na
kuwajali Waaandishi wa habari Erasto Ngole ameambatana na Viongozi wengine
Akiwemo Katibu Mpya wa umoja wa wanawake UWT mkoa wa Njombe,Katibu mpya UWT Wilaya ya
Njombe,Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe Angela Mwangeni,Mwenyekiti wa UVCCM Nehemia
Tweve,Katibu wa UVCCM mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti pamoja na pamoja na katibu
wa UVCCM Wilaya ya Njombe Daniel Mahanza pamoja na Afisa wa Vijana.
Badahi ya wanahabri walioambatana na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole katika Hafla fupi iliyofanyika Hillside Hotel. |
Akizungumza na wandishi wa Habari mara baada ya Chakula cha
Pamoja Erasto Ngole amewaomba Wandishi wa habari kuendelea kuutangaza mkoa wa Njombe na kuwafahamisha wananchi
kupitia vyombo vyao vya habari juu ya Namna Serikali ya Awamu ya Tano
ilivyodhamiria kuleta maendeleo na
huduma Muhimu za kijamii.
Chakula na Vinywaji havikukosekana |
Katibu Mwenezi CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole Pembeni ni viongozi wengine wa ccm |
Kadhalika Mh.Ngole amesifu Juhudi madhubuti zinazoendelea
kufanywa na Raisi wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake mzuri wa kuhakikisha anashughulikia Matatizo yaliyokuwa
yanawakabili Wananchi wa Mkoa wa Njombe
Ikiwemo Miundombinu ya Barabara.
Amesema Miongoni mwa Miradi Mikubwa inayotekelezwa mkoani
Nombe ni pamoja na Barabara ya Njombe-Ludewa hadi Manda, Barabara ya
Njombe-Makete hadi Mbeya,Barabara ya Kibena-Lupembe hadi Morogoro ambazo kwa
muda Mrefu zimekuwa haziwekewi Lami huku akishangazwa na utendaji kazi wa Raisi
Magufuli katika Kuhakikisha Nchi inafanikiwa katika Nyanja Mbalimbali.
Erasto Ngole aliyevaa suti ya kijivu bakiongea na Wandishi wa Habari ambao hawapo Pichani wengine ni Viongozi mbalimbali wa UVCCM na UWT Wilaya na Mkoa wa Njombe |
“Tunahakika barabara hizi kubwa nne zikikamilika tutakuwa
tumefanikiwa kwa asilimia kubwa sana kiuchumi kwani wananchi kwa mda mrefu
wamekuwa wakipata shida sana kusafirisha mazao yao,hivyo tuna kila sababu ya
kujivuni maendeleo haya yanayofanywa na Raisi Wetu Mpendwa John Magufuli”.Amesema
Ngole
Erasto Ngole amewambiwa wanahabari kuwa Chama cha mapinduzi
kinawategemea sana wanahabari hao kwani Vyombo vya habari vimekuwa na mchango
mkubwa sana katika jamii ya watu wa mkoa wa Njombe huku akiwataka kuwa
na umoja na kuondoa tofauti zao za kisiasa kwani maendeleo hayana Chama.
Katibu UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti akizungumza na Wandishi wa Habari,anaefuata ni Katibu mwewnezi Erasto Ngole na Mwisho ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe Angela Mwangeni |
“Sisi kama chama cha mapinduzi tunaimani sana na wandishi wa
habari wa mkoa wa njombe,nimewaita hapa leo kwa lengo la kukutana na nyinyi ili
tubadilishane mawazo kwani nyinyi wandishi wa habari ni kiuongo muhimu sana kati
yetu na wananchi,hivyo tunawaomba sana muwafahamishe wananchi juu ya mambo
makubwa yanayofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi Chini raisi Dokta John Pombe Magufuli”amesema
Ngole
Wa kwanza Kushoto Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe Angela mwangeni,Mwandishi wa Star Tv Dickson Kanyika na Katibu wa UVCCM wilaya ya Njombe Daniel Mahanza. |
Mh.Erasto Ngole ni Kiongozi mwenye Ari ya Kufanya kazi kwa Juhudi na Maarifa ambaye ana uwezo mkubwa katika
kuwatetea wananchi amesema anajisikia Faraja sana kukutana na wandishi wa
habari kwa siku ya leo kwani ni jambo ambao halijawahi kufanyika huko Nyuma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni