KATIBU MWENEZI CCM MKOA NJOMBE ERASTO NGOLE AWATAMBULISHA MAKATIBU WAPYA WA UWT MKOA NA WILAYA YA NJOMBE…..TEKRA MG’ONG’O ARITHI MIKOBA YA GRACE HAULE ALIYETEULIWA KUWA KATIBU WA UWT MKOA WA DAR ES SALAAM HUKU ANGELA MIREMBE AKIMRITHI MARY MIWA
Na.Erasto Mgeni ,Njombe.
Chama cha Maspinduzi mkoa wa Njombe Kimewatambulisha
makatibu wapya wa UWT Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Njombe ambao wamejaza nafasi
hizo zilizokuwa wazi.
Akiwatambulisha Mbele ya wanahabari Katibu wa Itikadi na
uenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole amesema anayofuraha
kumtambulisha Tekra Mng’ong’o aliyekuwa katibu Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Makete
akibadili nafasi iliyoachwa wazi na Grace Haule aliyeteuliwa kuwa katibu wa UWT
Mkoa wa Dar es Salaam
“mtakumbuka kwa,mba aliyekuwa katibu wetu Grace
Haule,aliyekuwa katibu wa UWT Wilaya ya Njombe baada ya kufanya kazi nzuri
iliyotukuka ameteuliwa sasa na mamlaka
kwenda kuwa katibu wa UWT Mkoa wa Dar Es Salaam na nafasi yake inachukuliwa na
Bi.Tekra Mg’ong’o.
Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti UWT Wilaya ya Njombe Angela Mwangeni,Katikati ni Katibu Mpya Mkoa wa Njombe Angela Mirembe na Mwisho katibu Mwenezi Erasto Ngole |
Kwa Upande Wake Bi Tekra ambaye ni mzaliwa wa Njombe na
mwenye Kipaji na umaarufu wa Kucheza
Mpira wa wavu(NetBall)amewaomba wanawake wa wilaya ya Njombe Kumuunga mkono
katika shughuli za Maendeleo.
“niwaombe sana akina mama wenzangu tulisongeshe mbele
gurudumu hili la maendeleo ambayo yanaletwa na chama cha Mapinduzi,Amesema
Bi.Tekra.
Wa kwanza kushoto ni Katibu Mpya wa UWT Wilaya ya Njombe Tekra Mg'ong'o,M/Kiti UWT W/Njombe Angela Mwangeni Katibu mpaya wa UWT Mkoa wa Njombe Angella Mirembe |
Hali kadhalika Katibu Mwenezi Erasto Ngole amesema
wamempokea katibu wa UWT Mkoa wa Njombe Bi Angela Mirembe aliyekuwa katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga akibadili
nafasi ya aliyekuwea katibu wa UWT Mkoa wa Njombe Bi Mary Miwa aliyepatwa na maradhi kutokana
na hali ya hewa ambaye aliomba uhamisho na sasa yuko mkoani Da Es Salaam.
Ngole amekishukuru chama cha Mapinduzi Taifa kwa kutambua
Pengo lililokuwepo katika nafasi hiyo kwani walikuwa wakifanya kazi kwa
Kuchechemea.
Katibu mpya wa UWT W/Njombe Tekra Mng'ong'o akiongea na wandishi wa habari |
“kwangu mimi kama mwenezi wa mkoa kitendo hiki nimekifurahia kwani tangu aondoke dada
yetu Mary Miwa tayari sekretarieti ya mkoa tulikuwa na upungufu mkubwa nahivyo
kazi zetu tulikuwa tukifanya kwa kuchechemea kwasababu timu ilikuwa
haijakamilika”
Baada ya Kutambulishwa Bi Angela Mirembe amewaomba waandishi
wa habari kushiriki kikamilifu katika kuwahabarisha wananchi wa mkoa wa Njombe
hasa katika kipindi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni