M/KITI UVCCM TAIFA Cde-KHERI JAMES AHUDHURIA UTIAJI SAINI UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Comrade Kheri James (MCC)
jana tarehe 03/9/2018 alihudhuria Shughuli ya Utiaji saini wa Mkataba
wa Ujenzi wa Meli mpya pamoja na ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv
Butiama katika ziwa Victoria.
Aidha
Mwenyekiti Kheri James Amempongea Mh Raisi Dkt John Pombe Joseph
Magufuli kwa kazi nzuri,kubwa na Juhudi zake za Kizalendo na Dhati
kabisa katika kuhaikisha anatekeleza ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI na
kuwaletea watanzania Maendeleo Kupitia Serekali ya awamu ya tano
UMOJA
WA VIJANA Utaendelea kumuunga mkono Mh Rais Dkt JOHN POMBE MAGUFULI na
Kusema mazuri yote yanayoendelea kufanywa na Serekali ya awamu ya Tano.
#TukutaneKazini
Imetolewa na:
Ndugu Hassan Bomboko
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni