NYUMBANI KWAZIDI KUNOGA!!!Madiwani Wengine Wawili CHADEMA Watimkia CCM.
Madiwani
hao walioshinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema, jana
usiku walitangaza kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM hivyo kufanya
idadi ya madiwani wa Arusha waliochukua hatua hiyo kufikia wanane.
Wakizungumzia
sababu za kujiuzulu, Alex Marti wa kata ya Olasitin na Amani Liwadi wa
kata ya Engutoto, wamesea lengo ni kumuunga mkono Rais John Magufuli.
“Nimeamua
kwa ridhaa yangu mwenyewe kujiuzulu udiwani. Nimeandika barua kwa
viongozi wa Chadema kueleza uamuzi wangu, kikubwa kilichofanya niamue
hivi ni kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli,” alisema Marti.
Liwadi pia alitoa sababu sawa na za Marti na kwamba tayari ameandika barua kwenda Chadema.
Uamuzi
huo wa madiwani hao unaifanya Chadema kubaki na madiwani 25, huku
madiwani wa CCM wakiwa saba kutoka idadi ya madiwani wawili
waliochaguliwa mwaka 2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni