Rais Magufuli Awataka Wanawake Wajifunze Tabia Njema Toka kwa Mama Maria Nyerere
Rais
Dkt. John Magufuli amewataka wanawake wote nchini wajifunze tabia njema
kupitia mama Maria Nyerere, kwa kile alichokieleza kuwa hajawahi
kuonyesha tabia ya tofauti tokea alivyokuwa na Hayati Mwl. Julius
Nyerere hadi hii leo.
Dkt.
Magufuli ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kwenye mkutano wa
hadhara katika uwanja wa Mwenge uliopo wilaya ya Butiama mkoani Mara,
muda mchache alipomaliza kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya
makutano Natta na Mugumu yenye urefu wa kilomita 135.
"Mama
Maria Nyerere wewe ni mama wa tofauti sana, ulivyokuwa na mzee wetu
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka ulivyo leo tabia yako
haijabadilika. Ni matumaini yangu wakina mama wengi watajifunza tabia
yako maana wapo wengine wakiolewa hata na muendesha daladala anabadilika
na wengine hata wakipata mwanaume mwenye kaduka hata hasalimii majirani
zake...
"Wewe
umekuwa mama wa taifa hili, wake wa viongozi wengi wanatakiwa wajifunze
kupitia kwako. Nimeona wake za viongozi wengi na wengine huwezi hata
kuwagusa. Wewe mama upo hivyo hivyo kama ulivyoletwa na Mungu hapa
duniani, hongera sana mama Maria Nyerere na ni kwasababu ya malezi
mazuri uliyoyapata", amesema Dkt. Magufuli.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo alivyokuwa anaeleza umma mambo mbalimbali
aliyoweza kuyafanya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere
ambaye amezikwa katika mkoa huo.
Mbali
na hilo, Rais Magufuli amesema Butiama ni sehemu ya historia ya nchi ya
Tanzania na hata kama watu watapinga hilo, lakini haitoweza kubadilika
jambo hilo.
Kwa
upande mwingine, Rais Magufuli amesema mara baada ya kuisha mradi wa
'stigler Gorge' itabidi ubadilishwe jina kuwa 'Nyerere Gorge', ili kumpa
heshima na kumuenzi Baba wa taifa ambae alitazama mbali juu ya
kufanyika kwa mradi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni