Dstv Tanzania

CCM KATA YA IBUMI YAENDELEA KUIFUATILIA SERIKALI.




Diwani wa Kata ya Ibumi wilayani Ludewa Mkoani Njombe Mh.Edward Haule ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Pamoja na Wataalamu wake wa Kata Wamefanya mikutano katika Vijiji vya Masimavalafu na Ibumi pamoja na Vitongoji vya Nyamalamba na Mkelema kwa lengo la Kuhamasisha Shughuli mbalimbali za Maendeleo kwa Wananchi.

Katika Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM Viongozi wa Chama hicho Kata ya Ibumi Walishiriki Mikutano Hiyo ili kufuatilia Utekelezaji wa Ilani na Kujionea Jinsi watumishi wa Serikali katika kata hiyo wanavyosikiliza na Kutatua Kero za Wananchi Vijijini.

Viongozi wa CCM walioshiriki Ziara hiyo Nipamoja na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Kata ya Ibumi Bw. Maiko Luoga Mwenyekiti Oddo s. Luoga Pamoja na Katibu wa CCM kata ya Ibumi Bw.Beda Mhagama.

Katika kijiji cha Masimavalafu Viongozi wametembelea Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho ambayo Umekamilika kwa Nguvu kubwa ya Wananchi, Serikali na wadau mbalimbali hivyo wananchi wa Kijiji hicho kwasasa wanaendelea na Ujenzi wa Nyumba ya Mganga ujenzi huo upo katika Hatua za Mwisho kukamilisha Ili Mganga aingie na Zahanati ianze Kufanya kazi Rasmi.

Aidha Diwani Mh.Edward Haule amehamasisha Ujenzi wa Vyumba Viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Ibumi kupitia Mpango wa TASAF kazi ambayo wananchi wameipokea vyema na wameshaanza Kuandaa Tofali za Ujenzi wa Madarasa hayo huku Diwani wao akijitolea Kuandaa jumla ya Tofali 5000 Wakati wananchi wakiandaa Tofali 500 Kila mmoja.

Mh.Edward Haule Diwani wa Kata ya Ibumi Ameendelea Kuhamasisha wananchi Kujituma katika Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata inayojengwa katika Kijiji cha Ibumi kwakushirikiana na Wadau Binafsi wa Village Schools Tanzania (VST) zoezi hilo lilishaanza wananchi wameandaa Mchanga, Tofali pamoja na Mawe Vifaa vingine vya Kiwandani vinatolewa na VST ujenzi huo ulishaanza kwasasa Shughuli mbalimbali Za Maendeleo zinaendelea.

Akiwa katika Mikutano hiyo iliyoanza October 06 hadi 08 Mwaka huu Diwani Edward Haule pamoja na Viongozi wa CCM Kata ya Ibumi Wamesikiliza Kero, Maoni, Ushauri Pamoja na Pongezi kwa serikali kutoka kwa Wananchi 37 waliopata nafasi katika Mikutano Ambapo Kero zimejibiwa.

Katika Kuboresha Michezo Diwani Wa Kata ya Ibumi Amekabidhi Mipira ya Mchezo wa Miguu kwa Timu za Ibumi, Nyamalamba na Mkelema Kufuatia Ombi maalumu la Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ibumi huku akiwataka Vijana Kukiunga Mkono Chama cha Mapinduzi na Serikali yake Pamoja na Kuwahimiza Vijana Hao kujituma katika Michezo ili Kukuza Vipaji vyao.

Imetolewa na Maiko Christopher Luoga Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Kata ya Ibumi 0762705839.

Hakuna maoni: