Dstv Tanzania

KATIBU MSTAAFU CCM MKOA WA NJOMBE HOSEA MPAGIKE (Mzee wa kanuni) AMKABIDHI OFISI YA CHAMA COMRADE PAZA MWAMLIMA


Pichani ni katibu wa CCM Mkoa wa Njombe akifanya mazungumzo na kamati ya siasa na secretarieti kabla ya kufanya makabidhiano


Katibu mstaafu CCM Mkoa wa Njombe Mzee Mpagige akiwa na wajumbe wa kamti ya Siasa na Sekretarieti Mkoa wa Njombe.
Amemkabidhi ofisi comrade PAZA MWAMLIMA ambaye amewasili Njombe kuvaa kiatu cha Mzee wa Kanuni.

Mzee Mpagike ambaye amekuwa mlezi wa jumuiya zote na kutoa miongozi mbalimbali yenye tija kwenye chama na kufanya chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe kukua kila siku na kufanya siasa safi ndizo zitawale katika Mkoa wa Njombe.

Katika makabidhiano hayo kamati ya siasa na secretarieti ya chama cha Mapinduzi wamesema watamkumbuka sana kwani alikuwa kiongozi wa kuigwa na kujivunia katika chama na jumuiya zote.

Hata hivyo mzee mpagike amewaomba viongozi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa kiongozi mpya aliyefika ili kufanya  chama cha mapinduzi kibaki kimbilio la watu wote.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano


Na Erasto Kidzumbe
0753580894




Hakuna maoni: