Dstv Tanzania

MNEC THERESIA MTEWELE AAGIZA UONGOZI WA KIJIJI KUWAIBUA WATOTO WALEMAVU ILI WAWEZE KUPATA ELIMU

Pichani ni Mjumbe wa Halmashauti kuu CCCM Taifa Theresia Mtewele, ameambatana na viongozi wa UVCCM (W) Iringa shule ya Msingi Kipera

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bi.  Theresia Mtewele amewataka viongozi na jamii kuwaibua watoto walemavu waliofichwa ili waweze kupata elimu ya msingi,  ameeleza kuwa kuwaibua huko kuendane na utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa kumsomesha mtoto mlemavu.

Ameyasema hayo katika mahafali  ya darasa la saba ya shule ya Msingi Kipera yenye mchanganyiko wa wanafunzi wenye mahitaji.


Aidha MNEC huyo amewaomba walimu kujikita katika elimu ya vitendo zaidi ili kuwasaidia wanafunzi kuwa na uelewa mzuri katika masomo yao.

Pia ametoa rai kwa wazazi na serikali ya kijiji kwa kuwalinda wahitimu na kuhakikisha wote wanakwenda sekondari mara tuu watakapochaguliwa.  Amewahimiza wanafunzi waendapo Shule ya sekondari wakasome kwa bidii ili waweze kufanikisha ndoto zao na kuongeza kuwa wajilinde na magonjwa ambukizi pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya.

MNEC ameitaka jamii kushirikiana kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu ili waweze kupata elimu kwani tatizo kwao ni pesa na si maarifa.  Katika kuunga hili ametahidi ufadhili kwa kuwaunganisha na wahisani wanafunzi wawili (2) waishio katika mazingira magumu wenye bidii ya kusoma kuanzia sekondari mpaka Chuo Kikuu.

MNEC pia amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kuthamini na kutoa mchango wao katika sekta ya elimu.

MNEC aliambatana na uongozi wa Umoja wa Vijana (UVCCM)  Wilaya ya Iringa Vijinini na Kaimu Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kalenga.




Hakuna maoni: