Dstv Tanzania

MJUMBE WA BARAZA KUU WAZAZI CCM MKOA WA NJOMBE NATHANAEL MAXONA AWAASA VIJANA WA MKOA WA NJOMBE KUSIMAMA NA FALSAFA YA TZ YA VIWANDA




Picha ni Mjumbe wa Baraza kuu wazazi mkoa wa Njombe Nathanael Maxona 

Akiwa katika kiwanda chake kidogo kilichopo Njombe Mjini nyuma ya jengo la CCM Wilaya ya Njombe.
Katika mahojiano na Stambuli Media amesema anaamini katika  Tanzania ya Viwanda, kwani ndiko fulsa nyingi za ajira zinapatikana na inawezekana  kujipatia kipato kirahisi.

Pamoja na hayo  amesema anawateja wengi katika kazi yake ya kutengeneza vifaa vya ujenzi na nyumbani. Jambo moja  la muhimu katika  kujiajiri ni kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uaminifu katika kazi.

Hata hivyo amesema kwa kadri anavyofanya kazi na kupata wateja wengi hajawahi fikiri suala la kuajiriwa kwani anauwezo wa kutengeneza fedha nyingi na kukidhi mahitaji yake muhimu ya familia ya kila siku ikiwa ataheshimu mambo matatu muhimu aliyo yataja hapo juu.

Mwisho amesema anaomba watanzania kwa pamoja tuijenge tanzania ya viwanda.



    Hizi ni moja ya kazi anazozifanya Nathanael Maxona










Hakuna maoni: