NAIBU KATIBU MKUU WA CCM TANZANIA BARA NDG. RODRICK MPOGOLO AKUTANA NA WAZEE WA WILAYA YA LIWALE.
Pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara
Ndg. Rodrick
Mpogolo
Ikiwa ni siku ya pili tangu alipoingia Wilaya ya Liwale,
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Ndg. Rodrick
Mpogolo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali ikiwemo
Mashina, Matawi na Kata ya Liwale Mjini.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 03/10/2018 kwenye
Ukumbi wa CCM Wilaya ya Liwale ambapo pamoja na mambo mengine mazungumzo
hayo yanalenga kukiimarisha Chama kuanzia ngazi ya Mashina kwani wanachama wengi wapo huko.
.
Wananchi wa Liwale watapiga kura tarehe 13/10/2018 amewaomba wananchi na wanachama kwa ujumla kumchagua Ndg. Zuber Mohamed Kuchaula ambaye ni mgombea toka CCM kwani ndiyo kiongozi atakaye waletea maendeleo na kutatua kero mbalimbali wanazokabiliana nazo wananchi wa Liwale.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni