MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA NJOMBE AMEHIMIZA WAZAZI KUPELEKA WATOTO SHULE
Pichani ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemeia Tweve.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe amewahimiza wazazi kupeleka watoto shule, amewahimiza alipo alikwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 4 ya Ufahamu Nursery School iliopo Njombe Mjini, akihotubia amesema hakuna sababu yeyote ile ya msingi ya kutopeleka watoto shule kwani Serikali
imeshabeba mzigo mzito wa kulipa ada.
Katika mahari hayo chipukizi waliohitimu ni takribani 72 ambapo ameahidi
vifaa vya michezo na kila mtoto atapata daftari 3 anapoenda kuanza
darasa la kwanza.
Aidha kauli mbiu ya mwenyekiti ni "Mwanzo
wa maisha bora ni Elimu Tanzania " amewaomba wazazi na wanachi kwa ujumla kupeleka watoto shule ndio hatma ya nchi yetu ya leo na kesho.
Mwisho amewambia wazazi hakuna nchi yeyote ile duniani ambayo imeendelea bila kujali suala la Elimu.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
MwenyeKiti akimkabidhi cheti chipukizi anayehitimu masomo ya nursery.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni